Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, May 22, 2015

AUNT EZEKIEL AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE, JINA LAKE COOKIE

AUNTY35Aunt Ezekiel


Ilikuwa si rahisi kama ilivyojulikana na wengi hasa kwa namna ya ‘fans’ wa staa wa filamu za Bongo maarufu  Bongo  Movie,  kujua  hatma ya ujauzito wake ambao ulikuwa ukifuatiliwa na wengi.  staa huyo si mwingine ni Aunty Ezekiel, katika kipindi chote cha ujauzito wake. Lakini kwa neema za Mungu, Asubuhi ya Mei 21.2015, staa huyo aliweza kuifungulia dunia kwa kumleta mtoto wa kike.
Hata hivyo, Mtoto huyo tayari jina lake limeshajulikana na anaitwa COOKIE.  Kwa sasa Aunt Ezekiel ni Mama Cookie na mtu wake  wa karibu aliyezaa naye ambaye ni Moses Iyobo  dansa wa Diamond Platnumz, kwa sasa anaitwa   Baba Cookie.
Mapema leo Mei 22, kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliandika ujumbe:
“Amin ktk Mungu ndio  Mwisho wa Matatizo  yote yaliyotuzunguka. Hakuna Mganga wala mchawi pasipo Mungu. Asante  Mungu wangu kwa kunikabidhi zawadi asubuhi ya jana tar 21-05-2015 Muache yy atende kwani ndio nguzo yetu sote Nasema Ahsante tena Ahsante kwa zawadi hii kubwa katika maisha  kwani ilikuwa ni kipindi kigumu chenye majaribu ya kila aina  kupitia  binadamu wajizaniao wao ni miungu watu Bac endelea kunyoosha mkono wako ktk paji la kiumbe wako ukiwa kama kinga nami niwe kivuli tuu juu yake.
Amen When Jesus Say Yes..  No body  can Say wht!!!!!! Wlcm Baby Cookie wlcm 2 da world KIBOKO YANG…LOVE!!” Aliandika Aunt Ezekiel kupitia ukurasa wake huo wa Instagram ambapo anatumia IG ya AuntyEzekiel.  Hata hivyo hadi sasa ujumbe huo umeweza kuendelea kupata LIKES na Comments nyingi ambazo karibu zote  fans wake wakimpongeza kwa kuweza kuifungulia dunia na kuleta mtoto.
aunty2 
Aunt Ezekiel akiwa na Moses Iyobo aliyezaa naye mtoto wao huyo aitwaye COOKIE!
Haya kazi kwako,kilicho baki ni kumuona Mtoto  COOKIE!!! Ambapo kila mmoja anashahuku ya kumuona mtoto huyo hivyo t unakuhakikishia kadri  tutakapopata  tutawaletea hapa. Pia  mtandao huu unatoa hongera kwa staa huyo  kwa kuweza kutuletea  ‘Aunty Cookie’

No comments:

Post a Comment