Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, April 19, 2015

Diamond Platinumz ‘kuwalipia’ Bima ya Afya wakazi 200 wa Tandale


10409754_830601046976768_7274119858185255012_nPost aliyotupia Diamondplatnumz kwenye mtandao wake wa Instagram. alipotembelea ofisi za Edgepoint Company Ltd watoaji wa huduma ya bima ya afya
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Kitu kingine kwa mwanamuziki anayefaanya vizuri Bongo nan je ya Bongo, Nasib Abdul maalufu kama Diamond Platinumz,  ameweza kuibuka nacho ni suala la kuisaidia jamii ya wakazi wa Tandale, eneo alilozaliwa na kukulia katika maisha yake.
Katika kurasa wake wa Instagram, Diamond Platinumz ama pia akifahamika kama Chibu Dangote, alitupia picha kadhaa alipokuwa katika ofisi za Edgepoit Company  Ltd huku akishukuru kwa kupatiwa Bima 200 za Afya kwa wakazi waTandale.
Kwa mujibu wa maelezo hayo, Diamond alibainisha kuwa, kampuni hiyo wamewezesha upatikanaji wa Bima ya Afya kwa wakazi 200 wa Tandale.  Bima hiyo ya Afya, ni ya mwaka mmoja ambayo itawawezesha wakazi hao watakaopatiwa bima hiyo kupata huduma katika Hospitali mbalimbali nchini.
11038561_830603376976535_7667024200917730253_nDiamond akiwa katika picha ya pamoja na mafisa wa Edge Point Comapany Ltd, alipotembelea ofisi hizo
Bima ya Afya inajishughulisha na utoaji wa bima ya afya kwa watu wote ikiwemo ya watu wa maisha ya kati na wasio katika ajira rasmi. Huku kwa wanaotaka kujiunga wanaweza kupiga *150*57# au 0714821422 au 0755885515.
Diamond ni kati ya wasanii wakubwa ambaye mara zote amekuwa mstari wa mbele kuisaidia jamii hasa katika makazi aliyokulia ya Tandale ambayo mara nyingi  kutokana na namna ya mazingira yake watu wengi ukiwaelezea Tandale wametokea kutokupapatia thamani lakini Diamond amekuwa akiheshimika na kutoa sifa mbalimbali ya maeneo hayo ya Tandale bila kuficha kama wafanyavyo wasanii wengine wanaojipa sifa za kuishi maeneo ya kitajili ikiwemo Masaki, Mbezi na Mikocheni.
988523_830601080310098_6372920903428271562_nUnapojiunga na bimaAFYA unakuwa na nafasi ya kupatiwa huduma bure katika hospitali mbalimbali karibu nchi nzima.
KWA HISANI YA MO BLOG

No comments:

Post a Comment