TIMU sita
zimefanikiwa kuingia kwenye hatua ya pili ya Ligi daraja la nne wilaya ya
Kilindi baada ya kumalizika hatua ya makundi.
Akizungumza
na kwa simu toka Kilindi, Katibu wa Chama cha Soka wilaya ya Kilindi, (KDFA),
Omari Javu alisema kuwa timu hizo zitaanza kumenyana katika hatua ya mwisho
Januari 5, katika Uwanja wa Mabobwe, Songwe mjini.
“Ligi
imefikia hatua ya mwisho na jumla ya timu sita zimefanikiwa kuingia hatua hii
na zitaanza kuchuana kwenye uwanja wa Mabobwe uliopo Songwe mjini.
Timu
zilizotinga hatua hiyo ni Kilindi FC na Dogodogo City toka kundi A la Songe
mjini, Mzalendo FC na Town stars toka
kundi B la Mafisa, Kiting FC toka kundi C la Kwekwizu na Tingisha FC toka
kundi D ambazo zitacheza kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Ligi hiyo
ilianza ikiwa na timu 14 na inachezeshwa
na waamuzi waliofuzwa sheria za soka na mkufunzi wa mkoa wa Tanga Damian
Mabena.
No comments:
Post a Comment