LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi ya tano kesho kwa mechi huku vinara Simba wakiwakaribisha Mbeya City kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Uwanja
wa Mkwakwani, Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting
Stars na Rhino Rangers ya Tabora. Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania
Prisons katika pambano litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine
jijini Mbeya.
Nayo
Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini
Bukoba kuvaana na Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi
itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara.
Ligi
hiyo itakamilisha mzunguko wa tano keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu)
kwa mechi tatu ambapo Azam na Yanga zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam
Complex.
Ruvu
Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa
mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment