Zimbabwe wameondolewa kushiriki Kombe la Dunia ambalo Fainali zake zitafanyika huko Russia Mwaka 2018.
Kamati ya Nidhamu ya FIFA jana imewajulisha ZIFA, chama cha Soka Zimbabwe, kwamba hawataruhusiwa kucheza Mashindano hayo ambayo wao walipaswa kucheza Mechi za Mchujo za Bara la Afrika ambalo hutoa Nchi 5 zinazocheza Fainali.
Kupigwa marufuku huku kumetokana na Nchi hiyo kushindwa kulipa Deni lao kwa aliekuwa Kocha wao Jose Claudinei Georgini.
Kocha huyo alilalamika kwa FIFA kupitia Kamati ya Hadhi za Wachezaji ambayo iluamuru Kocha huyo ana haki ya kulipwa.
Hata hivyo ZIFA ilishindwa kulipa Deni na Kocha huyo kwenda Kamati ya Nidhamu ya FIFA ambayo Aprili 2013 iliamua kuipiga Faini ZIFA na kuipa Siku 60 kulipa Nusu ya Deni na kulimaliza lote baada ya Siku 120.
ZIFA haikukata Rufaa kupinga uamuzi huo lakini vile vile hawakulipa Deni hilo katika muda waliopewa.
Ndipo FIFA, kupitia tena Kamati ya Nidhamu, kutoa tena Siku 60 lakini nazo zikapita bila Deni kulipwa.

No comments:
Post a Comment