YANGA wakiwa huko Sokoine Jijini Mbeya wamechukua usukani wa Ligi Kuu Vodacom baada ya kuitandika Tanzania Prisons Bao 3-0 wakati waliokuwa Vinara, Azam FC, ambao pia ndio Mabingwa Watetezi, kutoka Sare 0-0 na Ruvu Shooting huko Mabatini, Mlandizi, Mkoa wa Pwani.
Yanga sasa wapo kileleni wakiwa Pointi 2 mbele ya Azam FC huku Timu hizo zikiwa zote zimecheza Mechi 14 kila mmoja.
Bao za Yanga zilifungwa na Simon Msuva, Bao 2, na Mbrazil Coutinho aliepiga Bao 1 lakini yeye ndie Nyota wa Gemu baada ya kutengenezai Bao zote 2 za Msuva alieunganisha Kona zake mbili Dakika za 3 na 62.
Bao la Coutinho lilifungwa Dakika ya 11 na kusindikizwa wavuni na Beki wa Prisons katika harakati za kuokoa lakini Bao hilo linabaki kwa Mbrazil huyo kwa vile Mpira huo hata kama Beki huyo asingeugusa ulikuwa unatinga tu.
Hizi Mechi za Leo ni za viporo kwa Yanga na Azam Fcn na wote watatinga tena dimbani Jumapili kwa Yanga kubaki huko huko Sokoine Mbeya kucheza na Mbeya City na Azam FC kuwa kwao Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kucheza na Tanzania Prisons.
Jumapili hiyo hiyo ipo Mechi moja zaidi huko Kambarage, Mjini Shinyanga, wakati Stand United itakapoikaribisha Simba.
Lakini kabla ya hiyo Jumapili, Jumamosi zipo Mechi 3 za Ligi huko Miji ya Shinyanga, Mtwara na Tanga.
RATIBA/MATOKEO
Alhamisi Februari 19
Tanzania Prisons 0 vs 3 Yanga
Ruvu Shooting 0 vs 0 Azam FC
No comments:
Post a Comment