Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars), Rogasian
Kaijage ametangaza kikosi cha wachezaji thelathini (30) kitakachoingia kambini
siku ya jumapili kujiandaa na mchezo wa kufuzu Mataifa Afrika dhidi ya Zambia
mwezi Machi mwaka huu.
Kaijage ametangaza program yake ya
mazoezi itakayochukua takribani wiki nne (4) ili kuhakikisha wachezaji
wanakua tayari kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa kati ya Machi 21, 22 mwaka
huu, huku akipanga kucheza mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuelekea Lusaka
Zambia kwenye mchezo wa awali.
Twiga Stars ambayo itakua kambini katika Hosteli za Shirikisho la Mpira
wa Miguu nchini TFF zilizopo Karume, imeingia moja kwa moja katika hatua ya pili
kucheza na Zambia kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika msimamo wa viwango vya
soka la wanawake barani Afrika.
Wachezaji walioitwa ni, Asha Rashid, Esther Chaburuma, Fatuma Bushiri,
Fatuma Hassan, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi, Mwajuma Abdallah,
Sofia mwasikili, Zena Khamis, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu, Fadhira Hamad,
Anastazia Anthony, Shelder Boniface.
Wengine ni Thereza Yonna, Happines Hezron, Amina Ally, Donizia Daniel,
Fatuma Issa, Vumilia Maarifa, Maimuna Hamisi, Najiati Abbasi, Stumai Abdallah,
Ziada Ramadhani, Zuwena Aziz, Irene Joseph (Mfunzo – Zanzibar), Dawa Haji Vuai
(JKU – Zanzibar), Belina Julius na Amina Ramadhani.
No comments:
Post a Comment