Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 20, 2015

SOKA BEACH KAMILI KUIZAMISHA KENYA KESHO ESCAPE ONE

Wachezaji wa timu ya Taifa ya soka la ufukweni na makocha wao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye ufukwe wa Escape One jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa marudiano na Kenya wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za mashindano ya Mataifa ya Afrika zitakazochezwa nchini Shelisheli Aprili mwaka huu



Kocha wa timu ya Taifa ya soka la ufukweni, John Mwansasu akizungumza na wachezaji baada ya mazoezi yaliyofanyika Ufukwe wa Escape One jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa marudiano na Kenya wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za mashindano ya Mataifa ya Afrika zitakazochezwa nchini Shelisheli Aprili mwaka huu


TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) kesho itacheza mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya, mchezo utakaoanza majira ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Escape One Club Msasani jijini Dar es salaam.

Wageni timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni kutoka nchini Kenya wanatarajia kuwasili leo jioni jijini Dar es salaam, tayari kabisa kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano siku ya jumamosi na watafikia katika hoteli ya Saphire iliyopo eneo la Gerezani – Kariakoo.

Katika mchezo wa awali uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mombasa, timu ya Taifa ya Tanzania iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 5 – 3 dhidi ya wenyeji timu ya Taifa ya Kenya na kujitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele katika hatua inayofuata.


Waamuzi wa mchezo huo watakua ni , Beye Mbokh kutoka Senegal, mwamuzi wa pili ni Signate Youssouph (Senegal), mwamuzi wa tatu, Maolidy Tsaralaza kutoka Madagascar, mtunza muda (time keeper)  atakua Hachim Said Nassur (Madagascar) na kamishina wa mchezo atakua Roch Henriette kutoka Visiwa vya Shelisheli.

Tayari waamuzi wa mchezo huo wameshawasili jijini Dar e salaam tangu jana jioni tayari kwa mchezo huo, na endapo timu ya Taifa ya Tanzania itasonga mbele, itakutana na timu ya Taifa ya Misri kati ya Machi 7, 8 na kurudiana kati ya Machi 13, 14, 2015.

Fainali za Soka la Ufukweni zinatarajiwa kufanayika mapema mwaka huu katika Visiwa vya Shelisheli.

No comments:

Post a Comment