Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 27, 2015

TOTTENHAM HOTSPURS NA CHELSEA KUCHEZA FAINALI WEMBLEY CAPITAL ONE CUP JUMAPILI


MARA ya mwisho kukutana ni Mwezi uliopita Januari Mosi Uwanjani White Hart Lane kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na Tottenham Hotspur wakaibamiza Chelsea Bao 5-3 lakini safari hii Wikiendi hii wapo Wembley Jijini London kwenye Fainali ya Kombe la Ligi, Capital One Cup, hapo Jumapili.Siku hiyo ya Mwaka Mpya, Straika hatari na Chipukizi wa Tottenham Harry Kane, aliiongoza Spurs kwa kupiga Bao 2 na kutengeneza nyingine lakini Beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, amedai safari hii washapata dawa ya kuitandika Chelsea kwenye Fainali.

Ivanovic amedai Chelsea, ambayo itamkosa Kiungo wao Nemanja Matic aliefungiwa Mechi 2, inao uzoefu wa kucheza Fainali kupita Spurs.

Ametamba: “Tunajua nini tunapaswa kufanya. Ni Gemu ngumu lakini tupo tayari na tunaingojea kwa hamu!”

Tottenham wametinga Fainali baada ya kuitoa Sheffield United kwa Jumla ya Mabao 3-2 kwa kushinda Mechi ya Kwanza wakiwa kwao White Hart Lane 1-0 kwa Bao la Penati ya Andros Townsend na kisha kutoka Sare 2-2 katika Marudiano Nyumbani kwa Sheffield United.
Nao Chelsea walitinga Fainali baada ya kuifunga Liverpool 1-0 kwa Bao la Dakika za Nyongeza 30 la Branislav Ivanovic wakiwa Stamford Bridge baada ya Sare ya 1-1 katika Mechi ya Kwanza huko Anfield na kutinga Fainali kwa Jumla ya Mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment