Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 27, 2015

VAN GAAL ACHEKELEA TYLER BLACKETT KUSAINI MKATABA HADI 2017

MENEJA wa Manchester United Louis van Gaal ameeleza kufurahishwa kwake kwa kuweza kuongeza Mkataba wa Tyler Blackett hadi Mwaka 2017.
Mkataba wa Mchezaji huyo mwenye Miaka 20 ambae alianzia kucheza kwenye Chuo cha Soka cha Man United tangu akiwa na Miaka Minane ulikuwa umalizike mwishoni mwa Msimu huu.

Msimu huu Blackett aliibuka na kucheza kwa mara ya kwanza Timu ya Kwanza kwenye Mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu England dhidi ya Swansea na baadae kucheza Mechi 9. Ingawa Van Gaal hajampa namba tena Kinda huyo tangu Januari 11 lakini ni wazi Meneja huyo anamthamini sana.

Mara baada ya habari hizi za Blackett kuibuka, Van Gaal alisema: “Nimefurahishwa sana kwa Tyler kusaini Mkataba mpya. Yeye ni mmoja wa Wachezaji Chipukizi ambao Msimu huu wameweza kuchezea Timu ya Kwanza. Tyler ana uwezo mkubwa wa kuendelea zaidi na naamini yupo Klabu sahihi itakayokuza maendeleo yake na kuwa Beki bora!”

Blackett, ambae amekulia Kitongoji cha Hulme ambacho kipo Maili 2 tu toka Old Trafford, amesema: “Nimefurahishwa mno kusaini Mkataba mpya. Nimekuwa Shabiki wa United maisha yangu yote na nipo hapa tangu nina Miaka 8. Kuanzia Chuoni na kuweza kucheza Timu ya Kwanza ni ndoto iliyotimia. Nataka nijiendeleze zaidi na Timu ya Kwanza kwa msaada wa Meneja, Makocha na Wachezaji wenzangu.”

Mapema Mwezi huu, Kinda mwingine wa Man United ambae pia alianzia Chuo cha Soka cha Man United, Paddy MacNair, alipewa Mkataba mpya.

No comments:

Post a Comment