MAANDALIZI ya mashindano ya taifa ya mbio za nyika yatakayofanyika Arusha Jumamosi
yamekamilika na yanatarajia kushirikisha wanariadha kutoka mikoa yote ya
Tanzania.
Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui alisema kuwa,
mbio hizo za taifa za wazi ni kwa ajili ya kuchagua wachezaji watakaoingia
kambini kujiandaa na mbio za dunia za nyika zitakazofanyika China Machi 28.
Alisema kuwa muda wa mwezi mmoja unatosha kabisa kwa timu ya
taifa itakayochaguliwa kujiandaa kwa
ajili ya mashindano hayo ya dunia.
Nyambui alisema mkuwa
watachagua wachezaji sita badala ya watano ambao watagharamiwa na Shirikisho la
Kimataifa la Vyama vya Riadha (IAAF) ili kuwa na mchezaji mmoja zaidi katika
timu hiyo.
Alisema kuwa wachezaji watatatu wa kwanza ndio wanahesabiwa pointi
na wengine wawili ni mahsusi kwa ajili ya akiba endapo kuna mchezaji
atakayeumia, lakini wao wameongeza mmoja na kuwa sita.
Alisema kuwa ni matarajio yake mikoa yote itapeleka katika
mashindanohayo wachezaji walioandaliwa vizuri ili kupata timu bora
itakayofanyika vizuri katika mashindano hayo ya dunia.
No comments:
Post a Comment