Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 25, 2015

JKT RUVU YAIVIMBIA RED ARROWS KARUME





JKT Ruvu


Red Arrows

Benchi la Ufundi JKT Ruvu


Kushoto ni beki wa JKT Ruvu, Damas Makwaya akimzuia Ngoma Patrick wa Red Arrows ya Zambia kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa jana Uwanja wa Karume jini Dar es Salaam na timu kutoka sare ya 0-0
TIMU ya Red Arrows ya Zambia imelazimishwa sare ya bila kufungana na JKT Ruvu ya Pwani kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana.
Red Arrows ambayo inamilikiwa na jeshi ilijikuta ikikubali sare hiyo toka kwa wanajeshi wenzao wanaonolewa na kocha Minziro.
Mchezo huo ulianza kwa kasi huku kila timu ikijaribu kumsoma mpinzani wake ulinogeshwa na pasizilizojaa ufundi na macho na kufanya dakika 45 kuonekana chache.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambayo yalizidisha kasi ya mchezo lakini shukrani kwa mabeki wa timu zote kuwa imara na kufanya mpira uchezwe katikati kipindi chote cha pili
Red Arrows walionekana kujaribu kucheza shambulizi la haraka (counter attack) lakini mabeki wa JKT Ruvu walikuwa makini kuvunja mitego ya kuotea.
Baada ya mchezo huo kocha wa Red Arrows Mathew Phiri, alisema JKT Ruvu ni timu nzuri kwani hawachoki upesi na wachezaji ni wepesi kusoma mchezo jambo lililowafanya kushindwa kupenya ngome yao.
“Wapinzani wetu wa leo ni wepesi kusoma mchezo hivyo imekuwa rahisi kutubana tusiwafunge lakini pia wana nguvu na pumzi kuweza kuhimili dakika 90 bila kuchoka””, alisema Phiri
Naye kocha wa Kiluvya FC, Minziro alisema wachezaji wake wamecheza vizuri lakini hakuacha kuwasifia wapinzani wao kuwa wapo viziri kwenye utimamu wa mwili (physic) na kuongeza kuwa mchezo huo ni maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Machi 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam
Red Arrows kwenye mchezo wa awali iliifunga Kiluvya FC mabao 3-0 na ikafuatia kuifunga Ruvu Shooting bao 1-0 na jana kukubali suluhu.
Red Arrows wameondoka nchini jana baada ya kuweka kambi ya siku kumi kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Zambia inayotarajiwa kuanza Machi mwaka huu ambapo msimu uliopita ilimaliza ligi ikishika nafasi ya saba sawa na JKT Ruvu ilipo kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment