Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 25, 2015

COUNTINHO AACHWA YANGA



 
KIUNGO  wa Yanga, Andrey Coutinho ameachwa katika kikosi cha Yanga SC kilichoondoka Dar es Salaam kwenda Botswana kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya BDF XI kwa sababu ni majeruhi

Yanga SC wanatarajiwa kuwa wageni wa BDF Ijumaa wiki hii katika mchezo wa marudiano, raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na imeondoka na wachezaji 20 na viongozi saba

Yanga SC wanatakiwa  kulazimisha sare ugenini ili kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo baada ya mchezo wa awali kushinda mabao 2-0 jijini Dar es Salaam

Katibu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha amesema kikosi chao kimeondoka na wachezaji wote waliopitishwa na kocha wao Hans Pluijm.

Pia amesema kikosi chao kimeondoka na Ndege ya Shirika la Kenya  na wachezaji waliondoka ni  ni Ally Mustafa ‘Barthez,’ Deo Munish ‘Dida, Mbuyu Twite, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondani, Rajab Zahir, Pato Ngonyani, Salum Telela, Dilunga, Haruna Niyonzima, Mrisho Ngasa, Simon Msuva,Amissi Tambwe, Kpah Sherman na Danny Mrwanda

No comments:

Post a Comment