Kiluvya United ya Pwani na Njombe Mji ya mkoani Njombe ndizo timu
pekee zilizomaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa kushinda
mechi zote katika makundi yao, hivyo kujipatia pointi 15 kila moja.
Njombe Mji imeongoza kundi D lenye timu za Mkamba Rangers ya
Morogoro iliyofikisha pointi nane, Wenda ya Mbeya pointi sita, Volcano FC ya
Morogoro pointi sita, Town Small Boys ya Ruvuma pointi tano na Magereza ya
Iringa yenye pointi moja.
Katika kundi C, Kiluvya United inafuatiwa na Mshikamano ya Dar es
Salaam yenye pointi kumi, Abajalo pia ya Dar es Salaam pointi saba,
Cosmopolitan na Transit Camp za Dar es Salaam ambazo kila moja imemaliza
mzunguko huo ikiwa na pointi tano. Kariakoo ya Lindi haina pointi.
Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma na Singida United ya Singida ndizo
zinazochuana katika kundi A kila moja ikiwa na pointi nane. Mvuvuma FC ya
Kigoma yenye pointi tano ndiyo inayofuatia, wakati Milambo ya Tabora ina pointi
nne huku Ujenzi Rukwa ikikamata mkia kwa pointi moja.
Pia mchuano mkali uko katika kundi B ambapo JKT Rwamkoma ya Mara
na Mbao FC ya Mwanza ziko kileleni kila moja ikiwa na pointi tisa. AFC ya
Arusha inafuatia kwa pointi sita, Bulyanhulu FC ya Shinyanga ina pointi nne
wakati Pamba FC ya Mwanza iko mkiani kwa pointi moja.
Mzunguko wa pili wa ligi hiyo itakayotoa timu nne zitakazopanda
daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao (2015/2016) utaanza kutimua
vumbi Januari 24 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment