TIMU ya
Ashanti ya jijini Dar es Salaam juzi iliifundisha jinsi ya kusakata kabumbu
timu ya Kimondo FC ya Mbeya baada ya kuifunga mabao 5-3 kwenye mchezo wa Ligi
Daraja la Kwanza uliochezwa Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Kwenye
mchezo huo ambao ulikuwa umejawa na vituko toka kwa mashabiki wa Ashanti
ulishuhudia Kimondo wakipata bao la mapema kwenye sekunde 40 lililofungwa na
Peter Tweve aliyeunganisha mpira uliokuwa unagaagaa kwenye eneo la goli baada
ya mabeki wa Ashanti kutegeana kuuondoa.
Baada ya bao
hilo Ashanti walicharuka na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 14
lililofungwa na Seleman Sultan aliyewazidi mbio wachezaji wa Kimondo.
Dakika ya 34
Kimondo walipata bao la pili lililofungwa na Mpoki Mwakinyuke na Ashanti
walisawazisha dakika ya 36 bao likifungwa na Idd Seleman aliyefunga pia bao la
nne kwenye dakika ya 43
Kipindi cha
pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hali iliyosababisha mchezo kuwa
wa kasi na dakika ya 49 Kimondo walifanikiwa kuongeza bao lililofungwa na Mateo
Danny lakini Ashanti nao walisawazisha bao hilo dakika ya 66 lililofungwa na
mshambuliaji Moses Romward.
Ashanti
walifunga Karamu ya mabao dakika ya 87 baada ya Denis Omary kupiga mpira wa
faulo akiwa nje ya eneo la penati na kumpira kutinga wavuni moja kwa moja.
Katika hali
isiyotegemewa beki wa Ashanti, Mohamed Juma bega la mkono wa kushoto
lilichomoka hali iliyofanya madakatari wa huduma ya kwanza kumkimbiza hospitali
ya Amana na gari la wagonjwa ambalo lilikiwepo uwanjani.
Akizungumza
baada ya mchezo huo, kocha wa Ashanti Mbaraka Hassan aliwapongeza wachezaji
wake kwa ushindi walioupata na kusema kuwa ni zawadi tosha kwa mashabiki wao.
No comments:
Post a Comment