Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, October 10, 2014

ANGEL DI MARIA ADAI CRISTIANO RONALDO ALIMSHAWISHI AJIUNGE MANCHESTER UNITED

ANGEL DI MARIA amesema Cristiano Ronaldo ndie aliemshawishi kujiunga na Manchester United kutoka Real Madrid.
Man United ilivunja Rekodi ya Ada ya Uhamisho ya Uingereza walipoilipa Real Euro Milioni 75 kumnunua Staa huyo wa Argentina ambae aliichezea Real kwa Miaka Minne.
Di Maria sasa ametoboa kuwa Ronaldo ndie alikuwa na mkono mkubwa kwa yeye kufanya uamuzi wa kujiunga Man United ambako Ronaldo ndiko alikotwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani ya kwanza kwake na Msimu uliopita kuitwaa tena akiwa Real.
Andel Di Maria ameeleza: “Kabla hatujajua kama nitaenda Manchester aliniambia ni Klabu kubwa mno na nitakuwa na furaha huko na ni nzuri kwangu. Wakati huo hatukuwa na uhakika kama hili litatokea hivyo hatukuingia undani lakini alichoniambia kilinisaidia sana kutoa uamuzi wangu.”
Akiwa Man United, Ronaldo alivaa Jezi Namba 7 ambayo Kihistoria wanapewa Mastaa wakubwa huko old Trafford na waliowahi kuivaa ni pamoja na Malejendari George Best, Bryan Robson, Eric Cantona na David Beckham.
Alipotua Man United mwanzoni mwa Septemba, Angel Di Maria alikabidhiwa Jezi hiyo Namba 7 na mwenyewe ameeleza.
“Ni kichochea cha kunipa ari kubwa. Ukivaa Jezi iliyovaliwa na Watu kama David Beckham na Cristiano Ronaldo Siku zote utafurahishwa. Na ukweli kwamba Klabu imenipa Jezi hii inanipa imani kubwa na ndio maana nina furaha kuivaa!”
Akiongelea kuhusu Meneja Louis van Gaal, Di Maria amesema yeye ndio sababu nyingine iliyomfanya atue Old Trafford.“Tunaelewena vizuri sana. Yeye ni moja ya sababu nimekuja hapa. Ninashkuru sana alitaka kunisaini. Hilo linanifanya niwe na furaha.”
 Aliongeza: “Yeye ni Mtu anaetaka ushindi kila wakati na kuirudisha Klabu kwenye UEFA CHAMPIONS haraka iwezekanavyo hivyo tunao mkazo kwa hilo. Kila kipindi cha Mazoezi na kila Mechi tunataka kujitolea kwa Asilimia 100!”

No comments:

Post a Comment