
Bosi
wa zamani wa Argentina Alejandro Sabella amemtetea mshambuliaji Lionel
Messi akidai kuwa mshambuliaji huyo alijitoa kwa ajili ya taifa lake
katika fainali ya kombe la dunia nchini Brazil.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa katika mjadala mpana juu ya uwezo
wake alionyesha katika fainali hizo zilizopita huku Rais wa shirikisho
la soka duniani FIFA Sepp Blatter hapo jana akikaririwa akisema kuwa
mshambuliaji huyo hakustahili kushinda tuzo ya mpira wa dhahabu katika
fainali hizo
Hata
hivyo Sabella ameibuka na kudai kuwa Messi, ambaye ameshindwa kufunga
goli baada ya kufunga magoli manne katika michezo mitatu alijotoa kwa
kufanya kazi kubwa kwa ajili ya Argentina mpaka kuifikisha fainali
alipokubali kucheza katika nafasi ya juu kwa kuwasaidia wachezaji
wenzake.
"Messi ni mfano katika timu ya taifa," amesema Sabella mwenye umri wa miaka 59 alipokuwa akiongea na Radio La Red. "Alijitoa kimshikamano na wenzake
Sabella
aliachia ngazi kuifundisha Argentina muda mfupi baada ya fainali hizo
mjini Rio tangu kufikia mafanikio hayo ndani ya Albiceleste.
No comments:
Post a Comment