
Kwa upande wa Mameneja yupo pia yule wa Swansea City Garry Monk ambae ameiongoza Timu yake kushinda Mechi zao zote 3 za kwanza za Ligi na pia yuko Meneja wa Stoke City Mark Hughes ambae Timu yake iliwafunga Mabingwa Manchester City katika Mechi iliyopita huko Etihad.

Kwa upande wa Wachezaji yuko Straika wa Chelsea Diego Costa ambae ameifungia Timu yake Bao katika kila Mechi ya Ligi waliyocheza na pia yumo Kiungo wa Timu hiyo Cesc Fabregas ambae amekuwa aking’ara katika Mechi zote.

Wa mwisho kwenye Listi ya Wagombea kwa Wachezaji ni Mchezaji wa Aston Villa
Andreas Weimann ambae ameifungia Timu yake Mabao ya ushindi dhidi ya Stoke na Hull City
No comments:
Post a Comment