Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, September 12, 2014

RADAMEL FALCAO, DALEY BLIND WATAMBULISHWA RASMI MANCHESTER UNITED


WACHEZAJI WAPYA wa Manchester United, Radamel Falcao na Daley Blind, Leo hii wametambulishwa rasmi mbele ya Wanahabari huko Old Trafford Jijini Manchester United wakiwa pamoja na Meneja wa Klabu yao Louis van Gaal.
Falcao ndie aliejibu swali la kwanza na kusema: “”Nina furaha kubwa kuwa hapa. Ni changamoto kubwa katika maisha yangu ya Soka. Siku zote nimekuwa na ndoto ya kuwa kwenye Klabu kama Man United.” Akijibu swali aliloulizwa kuhusiana na kuumia vibaya Goti lake mwanzoni mwa Mwaka huu, Falcao, Mchezaji wa Kimataifa wa Colombia aliehamia kutoka AS Monaco kwa Mkopo wa Msimu mmoja ambao unaweza kuwa wa kudumu, alisema: “Najisikia vyema. Nilianza tena kucheza Miezi miwili iliyopita na Monaco na nimekuwa bora zaidi Mwezi uliopita na kufunga Mabao kadhaa ambacho ni kitu muhimu kwa Mastraika. Sina tatizo na Goti langu.”

Nae Blind, aliehamia kutoka Ajax na ambae alikuwa mmoja wa Wachezaji wa Van Gaal kwenye Kikosi cha Netherlands kwenye Kombe la Dunia, aliulizwa kuhusu uhusiano wake na Van Gaal na akasema: “Ni Mtu mkali na wa moja kwa moja. Wachezaji ni lazima wafuate kile kile ili kushinda gemu. Anasoma Mchezo vizuri na utabiri wake ulikuwa sahihi karibu kila Gemu kwenye Kombe la Dunia!”
Louis van Gaal aliulizwa atawezaje kupanga Wachezaji wote wapya kwenye Timu moja na akajibu: “Tumenunua Wachezaji watano. Mmoja ni wa Mkopo na pengine tutamnunua Msimu ujao-Falcao. Wachezaji 14 tumewaondoa na hivyo kupanga Wachezaji 6 wapya si tatizo wakati 6 wamebadilisha 14. Vile vile tutatumia Vijana!” Mechi ya kwanza kwa Wachezaji hawa wapya ni Jumapili Uwanjani Old Trafford kwenye Ligi Kuu England wakati Man United itakapocheza na QPR. Meneja Van Gaal akiwa na Radamel Falcao
Karibu sana Old Trafford! Radamel Falcao  akiwa kwenye nyasi za Uwanja wa Old Trafford
Wakipata darasa kutoka kwa Meneja Mpya Van Gaal Kocha Masidizi na mkongwe wa Old Trafford Giggs akiteta na Nahodha Wayne Rooney
Van Persie
Radamel Falcao kwenye mazoezi

No comments:

Post a Comment