UONGOZI wa Mkoa wa Soka wa Ilala, umesema kitendo cha timu
ya wanawake “Ilala Queens” kutinga robo fainali ya mashindano ya Taifa Cup si
cha kubahatisha.
Akizungumza jijini Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Ilala,
Daud Kanuti amesema Ilala wana wachezaji wazuri wenye kila sababu ya kutwaa
ubingwa wa Taifa Cup na kuwaomba wadau kuwapa sapoti.
“Ilala kuingia robo fainali si kwamba tulibahatisha bali ni
mbio za kuelekea nusu fainali na baadae na kulibakisha kombe ndani ya jiji la
Dar es Salaam kwani itakuwa aibu Dar es Salaam tuwe wanzishilishi wa ligi ya
wanawake halafu kombe liende mikoani”, alisema Kanuti.
Ilala imefuzu robo fainali baada ya kuifunga Mtwara queens
mabao 5-0 kwenye uwanja wa Karume na baadae kwenda kurudiana nao kwenye Uwanja
wa Nang’wanda Sijaona, Mtwara na kufungwa bao 1-0.
Mikoa mingine iliyofuzu kwenye robo fainali inayotarajiwa
kuanza kesho ni Kigoma, Mwanza, Pwani, Tanga, Temeke, Iringa na Mbeya na timu hizi zitawasili jijini
leo.
Taifa cup ya wanawake ni mashindano ya kwanza kufanyika
nchini na yanadhaminiwa na kampuni ya Proin na imeshirikisha mikoa yote
mwanachama wa TFF.
No comments:
Post a Comment