Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, September 12, 2014

UZINDUZI WA COKE STUDIO AFRICA WAFANA DAR


Wanamuziki Vanessa Mdee, Jo Makini na Shaa wakiwa katika picha ya pamoja kwenye 'red Carpet wakati wa uzinduzi huo. Habari na http://francisdande.blogspot.com/

Mwanamitindo Rio Paul (kushoto) akiwa na rafiki zake muda mfupi baada ya uzinduzi wa msimu wa pili wa Coke studio Africa, Hyatt Hotel, jijini Dar es Salaam.

Na Andrew Chale
Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, jana usiku ilizindua msimu wa pili wa onyesho la runinga lijulikanalo kama ‘Coke Studio Africa’ ambalo linatarajiwa konyeshwa kila Jumatatu na kituo cha Shirika la Utangazaji cha TBC.
Akizungumza na wandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt jijijini Dar es Salaam, Meneja bidhaa wa Coca-Cola Tanzania, Maurice Njowoka alisema, ni furaha na fahari kwa watanzania na waafrika kwa ujumla kwa kukutana pamoja na kuonyesha uwezo wa vipaji vyao hivyo, ambapo watu watapata kuona na kujifunza vipaji na radha nzuri kutoka kwa wasanii 24 wa bara la Afrika.

“Muziki ni lugha isiyo na mipaka na njia muhimu ya kuonyesha hisia na furaha, tungependa kusambaza furaha Barani Afrika kupitia muziki kwa kushirikiana na wasanii,” alisema Njowoka.

Alisema, ujumbe wa msimu wa mwaka huu ni ‘Ushirikiano wa Afrika, muziki wa afrika’, ambapo pia mbali na wasanii nyota pia wameweza kushirikisha bendi, watayarishaji muziki na madj bora wa bara la Afrika.

Njowoka aliwataja wasanii hao kwa mwaka huu na nchi zao kwenye mabano ni pamoja na Flavor Nabania, Omawumi, Waje, Burna Boy, Chidima, Olamide, Iyanya, Seyi Shay,Yemi Alade na Phyno (wote kutoka Nigeria), wengine ni Fena Gitu, Rabbit, Victoria Kimani na Jay A (Wote kutoka Kenya), Navio, Jacie Chandiru na Lilian Mbabazi (Kutoka Uganda), John Makini, Shaa, Diamond na Vanessa Mdee (Kutoka Tanzania).
Wengine ni Neyma, Jose Valdemiro na Marllen (Msumbiji) huku watayarishaji wa muziki ni Silvastone (Ghana), Chopstix na Afrologic (Nigeria), Kevin Provoke,Kagwe Mugai na Owuor Arunga (Kenya) na wengieo.
Hata hivyo, mbali na kuonyeshwa kila Jumatatu kupitia runinga ya TBC, mashabiki wanaweza kufuatilia pia kupitia tovuti ya Coke studio ambayo ni www.cokestudioafrica.com.
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na mastaa mbalimbali wakiwemo wanamitindo, wabunifu, mamiss, wasanii wa filamu, muziki, vichekesho.

No comments:

Post a Comment