Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 25, 2014

RAIS TFF KUFUNGA SEMINA YA UONGOZI NA UTAWALA KWA VIONGOZI WANAWAKE KESHO







RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Jamal Malinzi anatarajiwa kufunga semina ya uongozi na utawala kwa viongozi wa soka la wanawake Tanzania.
Semina hiyo ambayo ilianza Septemba 22 mwaka huu, inafanyika kwenye ofisi za Karume,  inashirikisha viongozi 46 wa soka la wanawake  kutoka mikoa yote wanachama wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
Akizungumza na gazeti hili msimamizi mwendeshaji wa semina hiyo, Mkufunzi Henry Tandau alisema kuwa lengo la semina hiyo ni kuwaweza viongozi wa soka la wanawake kuwa na uelewa wa jinsi ya kuendesha shughuli za kila siku zinazohusu soka kwenye mikoa yao.
“TFF imetoa semina hii ili kutoa mwanga wa jinsi ya kuongoza na kuendesha soka la wanawake kwenye mikoa yote ya Tanzania”, alisema Tandau.
Pia alisisitiza kuwa TFF imedhamiria soka la wanawake liende sambamba na soka la wanume ndio maana wameamua kuwaita viongozi wa soka la wanawake ili wakashirikiane na viongozi wa mikoa kuinua soka katika wilaya baadae ipatikane timu bora ya wanawake yenye sura ya kitaifa.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Wilfred Kidau alisema kuwa semina hii ni muhimu kwani itasaidia kuinua soka la wanawake ili liendane na nchi Nigeria, Afrika ya Kusini, Ghana na nyingine ambazo zimefanikiwa kwenye Nyanja ya soka la wanawake.
“Semina hii itasaidia kuinua soka letu liendane na wenzetu Afrika ambao wemeendelea kwani ina lengo la kuwasaidia kuibua vipaji, kutafuta wadhamini, kuandika pendekezo pia kujua kanuni zinazoendesha mashindano”, alisema Kidau.
Semina hii pia inawasaidia kwenda kusimamia kuandaa timu ambayo itashiriki ligi ya wanawake inayotarajiwa kuanza hivi karibuni, ligi ambayo itashirikisha mikoa yote wanachama wa TFF.

No comments:

Post a Comment