IKIWA
imebaki siku moja kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara, mambo tayari
yamenoga baada ya kukamilika kwa safu ya waamuzi watakaochezesha michuano hiyo
Jumamosi na Jumapili.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Silas Mwakibinga aliliambia gazeti hili
jana, orodha ya waamuzi iko tayari na kuwataka baadhi yao watakaochezesha
katika mchezo huo kutenda haki.
Katika
mchezo wa Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar ya pale Morogoro, mechi itakayopigwa kwenye uwanja wa Jamhuri
itachezeshwa na mwamuzi Dominick Nyamisano kutoka mkoani Dodoma.
Wakati huo,
wanalambalamba Azam FC itakuwa mwenyeji wa Polisi ya Morogoro kwenye uwanja wa
Azam Complex Chamazi, katika mchezo utakaochezeshwa na Mwamuzi Abdallah Kambuzi
kutoka mkoani Shinyanga.
Mchezo
mwingine utakaopigwa kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga kati ya Ndanda
Fc dhidi ya wenyeji wa mji Stand United itachezeshwa na Hashim Abdallah wa Dar
es Salaam.
Mchezo
mwingine utakuwa ni kati ya Mgambo dhidi ya Kagera Suger mchezo utakaopigwa
kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga na kuchezeshwa na Mwamuzi Kennedy Mapunda.
Aidha, Ruvu
Shooting itacheza na Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi na
kuchezeshwa na Mwamuzi David Paulo wa Mtwara.
Wakati huo,
Mbeya City ikiwakaribisha JKT Ruvu kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika
mchezo utakaochezeshwa na Mohamed Theophil.
Baada ya
mchezo huo wa Jumamosi, katika mchezo wa Jumapili watoto wa Msimbazi Simba
watakuwa ni wenyeji wa Coastal Union kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo mkazi wa mkoa wa Mara.
Mwakibinga
alisema anategemea waamuzi hao watachezesha mchezo huo kwa kufuata sheria 17 za soka, bila kupendelea na kwa
haki.
“Hiyo ndio
orodha ya kwanza, kuna nyingine itatoka kwani wapo wengi, na wasaidizi wao
tayari, tuna imani watazingatia maadili ya kazi yao,”alisema Mwakibinga.
No comments:
Post a Comment