Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, September 17, 2014

JKT RUVU YASHINDWA KUTAMBA KWA ASHANTI UNITED

Kocha wa JKT Ruvu, Minziro Felex


JKT Ruvu

Ashanti United





TIMU ya JKT Ruvu jana ilishindwa kutamba mbele ya Ashanti United baada kukubali suluhu kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.
JKT Ruvu ambayo ipo kwenye maandalizi ya Ligu Kuu huku Ashanti United wao wanajiandaa na Ligi Daraja la kwanza walianza mchezo huku kila timu ikifanya mashambulizi ya kushtukiza kwenye lango la mpinzani wake.
Ashanti ambayo imesheheni wachezaji chipukizi walionekana kuutawala mchezo huku wakipigiana pasi moja moja lakini umakini wa golikipa wa JKT Ruvu, Jackson Chove uliwafanya washindwe kufunga goli.
Kadri muda ulipozidi kuyoyoma kocha wa JKT Ruvu alikuwa akiwa himiza wachezaji wake wacheze kama alivyowafundisha vinginevyo wanataka kumuua.
“Nadir chezeni kama nilivyowafundisha jamani vinginevyo mnataka kuniua” alisikika Fred Felex Minziro akipiga kelele.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Fred Felex Minziro, alisifu kikosi chake kwa kandanda nzuri walioonyesha japo hawakuweza kupata goli.
“Wamecheza vizuri na naamini Ashanti United ni kipimo kizuri kwani ina wachezaji chipukizi ambao wanajua kutandaza soka hivyo naamini jumamosi nitaifunga Mbeya City”, alijigamba Minziro.
Timu hiyo imeondoka leo kelekea Mbeya kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

No comments:

Post a Comment