Wazee wa fedha: Makamu mwenyekiti wa United Edward Woodward (katikati), Joel Glazer (kushoto) na Richard Arnold (kulia) |
Manchester
United inatarajia kutangaza mapato yake ya mwaka hapo kesho ambao kiasi
cha pauni milioni £420 kitatangazwa ikiwa ni mapato yenye faida ya
pauni milioni £25 ambayo yametokana na uchapishaji wa jezi nakala
milioni .
Mapato
hayo ya mwaka yamejumuisha malipo ya meneja wa zamani David Moyes na
timu yake ya makocha, lakini kiasi hicho haki akisi hasara iliyotakana
na kushindwa kutinga katika michuano ya Ulaya msimu huu.
Tayari matokeo ya msingi yalikwisha kutolewa tangu mwezi Agosti katika soko la hisa la jijini New York(New York Stock Exchange).
Kitabu
cha taarifa kilichoandaliwa(Prospectus) kinaeleza kuwa mapato ya jumla
yanatarajiwa kuwa pauni milioni £429 mpaka pauni £434 ikiwa ni ongezeko
la asilimia 18 mpaka 19. Ikilinganishwa na Real Madrid iliyokuwa na
pauni milioni £480 lakini Real wakijumuisha mauzo ya wachezaji.
Faida
kwa mwaka inatarajiwa kuwa pauni milioni £23 mpaka milioni £25 ikiwa ni
chini anguko la pauni milioni £146.4 kwa mwaka 2012-13 lakini lakini
ikiwa ni baada ya kodi.
No comments:
Post a Comment