Kocha wa Nigeria, Stephen Kheshi
SHIRIKISHO la Soka Nigeria (NFF)
limetangaza kikosi cha cha awali cha wachezaji 30 kwa ajili ya Fainali
za Kombe la Dunia la FIFA nchini Brazil baadaye mwaka huu. Kutangazwa
kwa wachezaji hao jana, kumefutia kikao cha pamoja baina ya NFF na kocha
wa Super Eagles, Stephen Keshi.
Kikosi hicho ni makipa:
Vincent Enyeama, Austin Ejide, Chigozie Agbim na Daniel Akpeyi; Mabeki:
Elderson Echiejile, Juwon Oshaniwa, Godfrey Oboabona, Azubuike
Egwuekwe, Kenneth Omeruo, Joseph Yobo, Kunle Odunlami na Efe Ambrose.
Viungo: John
Mikel Obi, Ogenyi Onazi, Ramon Azeez, Joel Obi, Nosa Igiebor, Michael
Uchebo, Ejike Uzoenyi, Sunday Mba na Reuben Gabriel, wakati
washambuliaji ni: Ahmed Musa, Shola Ameobi, Emmanuel Emenike, Obinna
Nsofor, Osaze Odemwingie, Babatunde Michael, Victor Moses, Uche Nwofor
na Nnamdi Oduamadi.
Nigeria ni moja kati ya nchi tano za Afrika
zitakazoshiriki fainali za Kombe la dunia mwaka huu, pamoja na Algeria,
Ghana na Ivory Coast.
No comments:
Post a Comment