Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, April 14, 2014

LA LIGA: GETAFE 0 vs ATLETICO MADRID 2, FULL TIME! DIEGO GODIN & DIEGO COSTA WAIPAISHA KILELENI TENA ATLETICO USIKU HUU! DIEGO DA SIVA COSTA AUMIA!

Bao mbili za Diego Godín katika dakika ya 40 kipindi cha kwanza na lile la kipindi cha pili mwishoni kwenye dakika za lala salama la dakika ya 84 la Diego Costa zimeipa ushindi usiku huu timu Kinara Atletico Madrid.Mtanange huu ulikuwa mkali sana huku ukiwabakisha mtu 10 timu
ya Getafe baada ya mchezaji wake Lafita kumfanyia majanga Diego Costa na kupewa kadi  ya pili na nyekundu katika dakika ya 65 kipindi cha pili na kadi ya kwanza ya njano aliipata katika kipindi cha pili dakika ya 51.

Pamoja na Atletico Madrid kushinda waliopachika mabao yote mawili wote wamemaliza wakiwa na kadi za njano kila mmoja.

Pia Diego Costa alikosa mkwaju wa penati katika dakika ya 66 kipindi cha pili baada ya kipa wa Getafe kudaka mara mbili baada ya kuupangua mkwaju huo na mchezaji mwingine kupiga tena na kuuondosha nje ya lango.

Kipigo hiki pia kinawabakisha katika nafasi ya 18 chini ya mstari wa timu za kushuka daraja na ushindi kwa Atletico Madrid unawapaisha juu kwa pointi 82 wakifuatiwa na Real wenye pointi 79 na Barca wakishika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 79 baada ya kupoteza jana kwa kufungwa bao 1-0.Diego Costa mchezo huu umemwacha na majeraha

VIKOSI:
Getafe: Cordina, Alexis, Lago (Sammir 80'), Arroyo, Lopez, Lafita, León, Castro (Colunga 58'), Rodríguez, Mosquera (Lacen 68'), Marica
Goals: None.
Atlético Madrid: Courtois, Juanfran, Godín, Miranda, Luis, Suárez, Koke, García (Diego Rabas 71'), Gabi, Villa (López 62'), Costa (Rodríguez 86')
Goals: Godīn (40'), Costa (85')

No comments:

Post a Comment