Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 11, 2014

AFRICAN LYON YAJIWEKA PAZURI DARAJA LA KWANZA



TIMU ya African Lyon imejiweka katika nafasi nzuri ya kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga timu ya Villa Squad bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi daraja la kwanza uliochezwa Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani juzi.

Mchezo huo wa raundi ya pili ulikuwa wa ushindani kwani kila timu ilijitahidi kupambana walau iondoke na pointi tatu lakini hadi mapumziko hakuna timu iliyokuwa imeliona lango la mwenzake.

Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko lakini African Lyon ndio ilifaidika na mabadiliko hayo kwani dakika 70  ilipata bao lililofungwa na Mike Mbela

Akizungumza kwa simu kocha wa African Lyon Charles Otieno alisema kuwa anashukuru ameshinda mchezo huo kwani ulikuwa na ushindani na rafu za hapa na pale.

“Mchezo wetu na Villa ulikuwa mchezo mgumu lakini nashukuru wachezaji waliweza kufanya kile nilichowaelekeza kufanya na kufanikiwa kuondoka na pointi tatu”, alisema Otieno

Kwa matokeo hayo African Lyon imefikisha pointi  17 na mchezo ujao itacheza na Tesema kwenye Uwanja wa Karume, Ilala.

No comments:

Post a Comment