BONDIA
Francis Miyeyusho jana aliwapa raha ya kufunga mwaka watanzania baada ya
kumpiga kwa KO bondia Joshua Amakulu wa Kenya katika pambano lisilo la ubingwa
lililofanyika katika Ukumbi wa Msasani beach, Kinondoni.
Katika
pambano hilo Miyeyusho alimpiga Amakulu kwa KO raundi ya pili na kufanya ukumbi
ulipuke kwa nderemo na vifigo huku kila mtu akimpongeza Miyeyusho kwa kazi
nzuri ya kumpiga mpizani kabla ya kumaliza raundi zote 10.
Awali
Miyeyusho alikuwa apigane na David Charanga toka Kenya lakini bondia huyo
alifiwa na mama yake mzazi akalazimika kutofika ndipo akaja Amakulu aliyepokea
kipigo cha mbwa mwizi.
Katika
mapambano ya utangulizi bondia Ibrahimu Class 'King
Class alimpiga Mustafa Dotto kwa pointi katika pambano ambalo lilikuwa laraundi
sita
Bondia Kalama Nyilawila
alimpiga kwa KO kwenye raundi ya pili kwenye pambano la raundi
Bondia Iddy Mnyeke
na Cosmas Cheka walitoka sare katika pambano lililokuwa la raundi sita.
Akizungumza baada ya
mpambano huo Francis Miyeyusho alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kufanikiwa
kushinda pambano hilo pia kwa sapoti kubwa aliyoipata toka kwa viongozi na
mashabiki wa ngumi.
No comments:
Post a Comment