Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, January 20, 2014

ENGLISH PREMIER LEAGUE: LIVERPOOL ILIPOLAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA ASTON VILLA NYUMBANI

Steven Gerrard 53' PEN Daniel Sturridge 45' +2'  Andreas Weimann 25' • Christian Benteke 36


LIVERPOOL leo wametoka nyuma ya bao 2-0 na kusawazisha bao zote mbili katika kipindi cha kwanza na cha pili. Kipindi cha kwanza dakika za majeruhi dakika ya 45+ 2, Daniel Sturridge ameifungia bao na kwenda mapumziko zikiwa 2-1.Aston Villa bao zimefungwa na Andreas Weimann ambaye amefunga bao la kwanza katika dakika ya 25 na bao la pili likifungwa na Christian Benteke bao safi la kichwa baada ya mlinda mlango wa Liverpool kuukosa na mchezaji mwingine na hatimae Christian Benteke kumalizia bao hilo nyavuni katika dakika 36.
Dakika ya 53 kipindi cha pili liverpool wamepata bahati baada ya Suarez kujiangusha kwenye box na hatimaye Mwamuzi J. Moss kudai ni penati na mkwaju huo wa penati umefungwa na kapteni wa Liverpool Steven Gerrard. Sare hii inawabakisha hapo hapo katika nafasi ya nne Liverpool wakisubiri mtanange wa kesho kutwa jumatatu wa West Brom na Everton matokeo yake. Kama Everton watashinda watawaondoa katika nafasi hiyo ya nne.Katika kusaka pointi tatu muhimu....Brendan Rodgers (kulia), na Paul Lambert, wa Aston Villa Mmiliki wa Klabu ya Liverpool John Henry nae alikuwemo uwanjani kuwacheki vijanaMmiliki wa Klabu ya Liverpool John Henry aliambatana na mama Linda Pizzuti Suarez akiendesha....Kawaida kwa Suarez!!Suarez alinyanyuka na kuendelea na kipute kama kawa!!Christian Benteke na leo amefunga bao na hapa alikuwa anashangilia bao hilo2-0: Kila kocha akitoa maelezo sasa!! nini kifanyike na kipi kiendelee
Raheem Sterling akimvuta jezi mchezaji wa Villa FabianSuarez alianguka ndani ya box akiwa na kipa wa Villa Guzan na mwamuzi kusema ni penatiSteven Gerrard akifunga mkwaju huo wa penatiPenati ndio unaweza ukasema imewaokoa liverpool leo

MATOKEO YA MITANANGE YA LEO JUMAMOSI:
Jumamosi Januari 18

Sunderland 2 v Southampton 2
Arsenal 2 v Fulham 0
Crystal Palace 1 v  Stoke 0
Man City 4 v Cardiff 2
Norwich 1 v Hull City 0
West Ham 1 v Newcastle 3
Liverpool 2 v Aston Villa 2

No comments:

Post a Comment