


Samuel Eto'o akifunga bao mpira uliotenguliwa na Michael Carrick na hatimaye kuingia langoni mwa United.
Dakika ya 17 Samwel Eto'o anaipatia bao Chelsea na kufanya 1-0 dhidi ya Man united. Bao la pili Samwel akaiongezea tena bao Chelsea katika dakika za mwishoni za kipindi cha kwanza akifunga katika dakika ya 45. Bao la tatu ni la Eto'o tena..

Mzee Ferguson akishuhudia bao 2-0 za Chelsea hapa katikati ya mashabiki.



Chelsea walipata Bao lao la kwanza katika Dakika ya 17, bila kutegemewa kwani Man United ndio waliokuwa juu kimchezo, baada ya uzembe wa kutomkaba Samuel Eto'o ambae alipokea Mpira wa kurushwa na kumhadaa kirahisi Phil Jones kisha kupiga Shuti la Mita 20 na kumbabatiza Mchael Carrick na kumpoteza Kipa De Gea.
Bao la Pili lilifungwa kwenye Dakika ya 45 na Eto’o kufuatia ulinzi duni baada Kona kupigwa na kuokolewa na Mpira kumkuta Ramires aliempasia Cahill aliemsogezea Eto’o na kupachika kilaini.

Bao la 3 lilipigwa tena na Eto’o, ni Hetitriki kwake, kufuatia Kona ya Dakika ya 49 iliyounganishwa na Cahill na kuokolewa na De Gea na kutua miguuni mwa Eto’o ambae alimalizia kilaini kwa mara nyingine.
Javier Hernandez ‘Chicharito’ aliifungia Bao lao pekee Man United katika Dakika ya 78 kufuatia kazi njema ya Danny Welbeck kumfikia Phil Jones ambae shuti lake lilionekana kutokuwa na madhara hadi alipochomoza Chicharito.
Man United walimaliza Mechi hii Mtu 10 baada Nahodha wao Nemanja Vidic kupewa Kadi Nyekundu kwa Rafu mbaya kwa Eden Hazard.






Eto'o akishangilia baada ya kufunga bao la pili hapa.

Majanga: Januzaj na Danny Welbeck wakilianzisha baada ya kufungwa bao na Samwel












Eto'o akipokea pongezi kutoka kwa viongozi wake kwenye bench
Eto'o akifanya yake mbele ya Camera!!
Gary Cahill akishangilia...
Moyes ...
David Beckham hakuwa na furaha
Roman Abramovich
Petr Cech chupuchupu afungwe na Javier Hernandez...
Antonio Valencia...
Javier Hernandez akishangilia bao lake katika dakika ya 78
Nemanja Vidic kalambiswa kadi nyekundu
Nemanja Vidic nje!!!








Javier Hernandez akishangilia bao lake katika dakika ya 78


VIKOSI:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Luiz, Willian (Matic 85'), Oscar (Mikel 67'), Hazard, Eto'o (Torres 78').
Subs not used: Cole, Lampard, Mata, Schwarzer.
Booked: Luiz
Goals: Eto'o 17', 45', 49'
Man Utd: De Gea, Rafael Da Silva, Evans, Vidic, Evra (Smalling 61'), Jones, Carrick, Valencia, Januzaj, Young (Hernandez 56'), Welbeck.
Subs not used: Giggs, Lindegaard, Cleverley, Fletcher, Kagawa.
Booked: Young, Valencia
Sent off: Vidic
Goal: Hernandez 78'
Referee: Phil Dowd
Subs not used: Cole, Lampard, Mata, Schwarzer.
Booked: Luiz
Goals: Eto'o 17', 45', 49'
Man Utd: De Gea, Rafael Da Silva, Evans, Vidic, Evra (Smalling 61'), Jones, Carrick, Valencia, Januzaj, Young (Hernandez 56'), Welbeck.
Subs not used: Giggs, Lindegaard, Cleverley, Fletcher, Kagawa.
Booked: Young, Valencia
Sent off: Vidic
Goal: Hernandez 78'
Referee: Phil Dowd
No comments:
Post a Comment