BONDIA Francis Cheka juzi alichezea
kichapo cha KO kutoka kwa Fedor Chudinov wa Russia na kuvuliwa rasmi mkanda wa
WBF alioupata baada ya kumpiga bondia Phil Williams wa Marekani kwenye pambano
la lisilokuwa na ubingwa la raundi 8.
Mpambano huo ulifanyika nchini
Russia katika Ukumbi wa Dynamo Palace of Sports in Krylatskoye ni wa kwanza
kuchapwa baada ya kutawazwa kuwa bingwa wa WBF, mkanda ambao anaushikilia lakini kutokana na sheria za WBF ukipigwa kwa
KO kwenye mpambano wa kirafiki unapoteza mkanda huo.
Kwa kipigo hicho Cheka ameporomoka
kwenye viwango vya ubora vya WBF toka nafasi ya 20 hadi 48 na inamlazimu
kufanya kazi ya ziada kuhakikisha kuwa anaomba kugombea mkanda wa WBF kabla ya
Januari mwakani.
Akizungumza kwa masikitiko promota
J. Msangi alisema kuwa Cheka hakupaswa kupigana mapambano kama hilo kwani
alikuwa hajajiandaa vya kutosha nab ado yeye alikuwa anamwandalia pammbano
ambalo angepigana Februari, mwakani.
“Cheka alipokuwa amefikia hakupaswa
kupigana mapambano ya kulipwa dola 10,000, kwa sasa yeye anatakiwa kupigana
pambano ambalo anatakiwa kulipwa kuanzia dola 30,000 hadi 60,000 lakini
nimesikitika zaidi baada ya kusikia kapigwa kwa KO raundi ya tatu na kupoteza
mkanda wake”, alisema Msangi.
Pia Msangi alisema kuwa
watawasiliana na WBF kuomba Cheka agombanie
huo mkanda hapa nchini mapema Januari 24, mwakani ili iwe rahisi kwake
kushinda kwani kwa sasa huo.
Katika pambano hilo bondia mwingine
wa Tanzania Allan Kamote naye alipigwa kwa KO raundi ya 7 kwenye pambano ambalo
lilikuwa la raundi tisa.
Taarifa zilizopo kwa mwaka huu
mabondia 16 waliokwenda kucheza nje ya nchi hakuna hata mmoja aliyeshinda jambo
ambalo linaacha maswali mengi kwa wadau wa ngumi
No comments:
Post a Comment