Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, December 23, 2013

JAPHET KASEBA AMPIGA ALIBABA RAMADHAN KWA KO JANA





Bondia Japhert Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Alibaba Ramadhani wakati wa kugombania ubingwa wa Taifa uliofanyika Manzese Dar es salaam Kaseba alishinda kwa KO ya raundi ya nne ya mpambano huo
Kanda kabongo akimuhuumia Japhert Kaseba
Bondia Omari Nampekecha 'peche boy' kushoto akipambana na hasani Kiware wakati wa mpambano huo nampekecha alishinda kwa pointi
Bondia Pendo Njau kushoto akiwa na bondia Llulu Kayage wakati wa mpambano huo
Wapiganaji wa mpambano wa Kick Boxing Kareem Kutch (kushoto) akipambana na Hassani Juma 'Tata Boy' wakati wa mpambano huo kutch alishinda kwa pointi
Wapiganaji wa mpambano wa Kick

BONDIA Japhet Kaseba juzi alitawazwa kuwa bingwa wa Taifa baada ya kumpiga kwa KO bondia Alibaba Ramadhan wa Arusha kwenye raundi ya nne katika pambano lililokuwa la raundi 10 lililofanyika Ukumbi wa Friends Corner Manzese, Dar es Salaam.
Kaseba ambaye awali alikuwa akipigana ngumi na mateke kabla ya kuhamia kwenye ngumi tu alionyesha umahiri wake wa kupiga makonde mazito ambayo yalionekana kumwelemea Alibaba.
Katika kuonyesha kuwa yeye yupo fiti Kaseba aliendelea kumrushia makonde mfululizo mpinzani wake na kusalimu amri katika raundi ya nne.

Katika pambano la ngumi na mateke (Kick Boxing) Kareem kutch alimshinda kwa pointi Hassan Juma 'Tata Boy’ kwenye pambano la raundi nne.

Akizungumza baada ya pambano hilo, Japhet Kaseba alisema kuwa anashukuru kwa kumpiga Alibaba Ramadhan na kufanikiwa kupata mkanda wa Ubingwa Taifa.

“Nashukuru Mungu kwa kutwaa ubingwa wa Taifa hivyo mkanda huu unanipa chachu ya kuendelea kujifua vema ili kugombea mikanda mingine”, alisema Kaseba.

Naye mwandaaji wa pambano hili Mkurugenzi wa BigRight Promotion, Ibrahim  Kamwe aliwashukuru wadau wa ngumi kwa kumuunga mkono kwa wingi kwani bila wao asingeweza kuandaa pambano hilo.

“Nawashukuru mabondia wote na wadau kwa kunipa sapoti kwani bila wao nisingeweza kuandaa mapambano haya hivyo  nawaomba waendelee kutusapoti kwani kwa kufanya hivyo wanausadia mchezo wa masumbi”, alisema Kamwe

No comments:

Post a Comment