Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, November 3, 2013

MASHAUZI CLASSIC KUPAMBA USIKU WA KANGA ZA KALE NOVEMBA 8 SERENA

usiku wa khanga za kale 2013
Na Andrew Chale
Onesho  la  Usiku wa Khanga za Kale 2013, maarufu kama ‘5th Extra Vaa Khanga Party’ linatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam usiku wa Novemba 8, kwenye Hoteli ya Serena na kupambwa na burudani ya nguvu kutoka kwa bendi ya Mashauzi Classic.
Mwandaaji wa onesho hilo, Asia Idarous Khamsin,  amesema tayari maandalizi yake yamekamilika na amewasihi wadau kujitokeza kwa wingi katika onesho hilo la aina yake kujionea mitindo mbalimbali ya khanga.
“Wadau wa mitindo nchini, watapata burudani na kufurahia mitindo ya khanga itakayooneshwa kwenye shoo hiyo, hii si ya kukosa kwa mwaka huu,” amesema Asia Idarous.
Amesema usiku huo, vazi la Khanga  ndilo litakuwa maalumu  kwa wadau watakaohudhuria sambamba na kupinga matumizi ya dawa za kulevya.
Onesho la Usiku wa Khanga za Kale 2013, ambalo mwaka huu limeandaliwa kwa ushirikiano wa Asia Idarous Khamsin na Fabak Fashions, linatarajiwa kuwa na shangwe mbalimbali ikiwamo kushirikisha watu maarufu na mastaa mbalimbali.
Kuhusu kiingilio, Idarous alisema kwa viti vya kawaida ni sh 30,000 na viti maalumu itakuwa ni sh 50,000 na kuongeza kuwa tiketi zimeanza kuuzwa Fabak Fashions Mikocheni na Gift Shop Serena Hoteli.
Amefafanua kuwa onesho hilo linafanyika chini ya uwezeshaji wa wadhaminiwa kama bia ya Redd’s, CXC, Clouds FM, Vayle Spring, Magic FM, Eye View, Amina Design, Kabile, Voice of America, Origin Unite, Channel Ten, DTV, Times FM, Michuzi Media Group, Event Light na Miss Tz.

No comments:

Post a Comment