WAJUMBE kutoka nchi 54
ambao ni wanachama wa Shirikisho la Soka barani Ulaya wameunga mkono mpango wa
kuhamisha michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar
kuchezwa katika majira ya baridi baada ya kukubaliana kwamba haitawezekana
michuano hiyo kuchezwa katika majira ya kiangazi kama
ilivyo kawaida.
Makamu wa rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Jim Boyce
alithibitisha kuwa jambo walilokubaliana katika mkutano huo ni kwamba Kombe la
Dunia nchini Qatar
haliwezi kuchezwa katika majira ya kiangazi.
Hata hivyo Boyce aliongeza
kuwa kila mtu amekubaliana na hilo
lakini ni tarehe halisi ya kuhamisha michuano hiyo ndio hawajafikia maamuzi
yake.
Suala la michuano hiyo kuandaliwa majira ya kiangazi nchini Qatar limekuwa
likizua mjadala mkubwa kutokana na joto kali katika kipindi hicho linaloweza
kufikia nyuzi joto 50.
Kamati ya Utendaji ya FIFA inatarajiwa kukutana
Octoba 3 mwaka huu huko jijini Zurich,
Switzerland ili
kujadili mapendekezo ya kuhamisha michuano hiyo katika majira ya baridi.
No comments:
Post a Comment