VIPIGO
mfululizo kwa Jose Mourinho na Chelsea yake vimepokewa kwa vicheko na
wapinzani wake huko Spain ambako Meneja huyo wa Chelsea aliishi na Real
Madrid na kujitumbukiza katika utata na migogoro kibao.
Wakati Klabu yake ya zamani Real Madrid
ikisheherekea ushindi wa Ugenini wa Bao 6-1 walipoitwanga Galatasaray
huko Uturuki hapo Jumanne kwenye Mechi ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ
LIGI, UCL, Jose Mourinho alijikuta akiangukia pua kwa kubandikwa Bao 2-1
na FC Basel kwenye Mashindano hayo hayo Siku ya Jumatano tena Uwanjani
kwao Stamford Bridge.
Na hicho kilikuwa kipigo cha pili
mfululizo kwa Jose Mourinho ambae Wikiendi iliyopita alibutuliwa Bao 1-0
na Everton kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Hali hii imeleta vicheko huko Spain na
baadhi ya kejeli ni Mabango: “Itachukua muda gani kabla hajambenchi Petr
Cech!” na “Hana lolote bila Aitor Karanka!”
Mabango hayo yalikuwa yakimaanisha jinsi
alivyompiga Benchi Nahodha na Kipa Nambari Wani wa Real na Spain, Iker
Casillas, na ile tabia yake mambo yakiwa magumu kwake kumtuma Msaidizi
wake Aitor Karanka kuongea na Wanahabari.
Lakini huko Nou Camp, kwa watani wa
Mourinho alipokuwa Real, Mchezaji wa Barcelona, Gerrard Pique, ambae
alifunga Bao moja wakati Timu yao inaichapa Ajax 4-0 kwenye UCL,
aligusia kichapo cha Chelsea kwa kusema: “Kwenye Makundi ni lazima
ukwepa kushangazwa! Chelsea, kufungwa na Basel Nyumbani, ni mfano huo na
hilo linaleta mambo magumu.”
UEFA CHAMPIONS LEAGUE
MATOKEO:
Jumanne 17 Sep 2013
Manchester United FC 4 Bayer 04 Leverkusen 2
Real Sociedad de Fútbol 0 FC Shakhtar Donetsk 2
Galatasaray A.Ş. 1 Real Madrid CF 6
FC København 1 Juventus 1
SL Benfica 2 RSC Anderlecht 0
Olympiacos FC 1 Paris Saint-Germain 4
FC Bayern München 3 PFC CSKA Moscow 0
FC Viktoria Plzeň 0 Manchester City FC 3
Jumatano 18 Sep 2013
FC Schalke 3 FC Steaua Bucureşti 0
Chelsea 1 FC Basel 2
Olympique de Marseille 1 Arsenal 2
SSC Napoli 2 Borussia Dortmund 1
FK Austria Wien 0 FC Porto 1
Club Atlético de Madrid 3 Football Club Zenit 1
AC Milan 2 Celtic FC 0
FC Barcelona 4 AFC Ajax 0
No comments:
Post a Comment