MENEJA
MSTAAFU wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amevunja ukimya wake
na kuzungumza kwa mara ya kwanza kuhusu Wayne Rooney tangu adai Mwezi
Mei kuwa Mchezaji huyo anataka kuihama Klabu hiyo.
Soma Zaidi Hapa »
You might also lik
Ferguson, ambae
alistaafu mwishoni mwa Msimu uliopita na nafasi yake kuchukuliwa na
David Moyes lakini amebaki Klabuni hapo kama Mkurugenzi, Msimu huu
amehudhuria Mechi mbili za Man United walizocheza Old Trafford dhidi ya
Crystal Palace kwenye Ligi na ile ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Jumanne Usiku
walipoifunga Bayer Leverkusen ya Germany Bao 4-2 na Rooney kupachika Bao
2.
Akiongea na Kituo cha TV cha Man United, MUTV, Ferguson alisema: “Rooney alikuwa hatari, nguvu yake imerudi, ari yake na nia ya kushambulia. Nikiwa Mkurugenzi, nimefurahi kumuona akicheza vizuri. Amerudi pale ambako sote Siku zote tunapakumbuka.”
Kauli hii ya Ferguson inachukuliwa kama ni ya makusudi ya kumfanya Staa huyo atulie baada ya kusakamwa na nia ya kuhama ikidaiwa kauli ya Mwezi Mei ya Feguson kwamba Rooney anataka kuhama ndio ilimfanya Straika huyo asiwe na furaha Klabuni na kuanza kuandamwa na Chelsea wakimtaka aende kwao.
Hadi hii leo Rooney mwenyewe hajatamka lolote kuhusu sakata hili mbali ya kuwashukuru Mashabiki wa Man United kwa kumpa sapoti kubwa.
Kufuatia kustaafu kwa Ferguson na kuja kwa David Moyes, ambae ndie alimpa nafasi Rooney alipokuwa nae Everton, kuchomoza na kucheza Soka la Timu ya Kwanza wakati akiwa Kinda, pia kumetuliza msuguano huo na Rooney na sasa ipo mikakati ya kuboresha Mkataba wa sasa wa Mchezaji huyo ambao unamalizika Mwaka 2015.

No comments:
Post a Comment