TIMU ya soka ya mkoa wa Ilala leo
imetoka sare ya
mabao 3-3 dhidi ya mkoa wa Kaskazini Unguja katika mchezo wa ufunguzi wa
mashindano ya Copa Cocacola uliochezwa kwenye uwanja wa shirika la elimu
Kibaha, Pwani.
Timu ya
Ilala ndio ilikuwa ya kwanza kuona lango la wapinzani wao katika dakika ya 10
kupitia kwa mshambulaji wake Ally Shabani baada ya kuwazidi mbio mabeki wa
Kaskazini Unguja na dakika 35 Ally alifunga bao la pili .
Kipindi cha
pili kikianza Ilala wakiwa mbele kwa bao 2-0 lakini Unguja Kaskazini walifanya
shambulizi na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Usi Makame dakika ya 49 kwa penati baada ya beki
Jamal Akida kunawa mpira katika harakati za kuondoa mpira eneo la hatari.
Baada ya
hapo Ilala walijitahidi kuongeza bao na dakika ya 49 kupitia kwa mshambuliaji
wake Harun Said.
Katika
dakika ya 64 Shaban Ada wa Ilala
alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumkwatua Faki Juma wa Unguja
Kaskazini.
Baada ya
kadi nyekundu, Unguja Kaskazini
walizinduka na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 64 kupitia kwa Jecha Juma.
Unguja
Kaskazini waliendelea kuliandama lango la Ilala na dakika 78 walipata penati
baada ya Jamal Akida wa Ilala kumkwatua
Haji Makame na Jecha Juma kufunga bao la tatu na kufanya matokeo kuwa 3-3
Mchezo huo
ambao ulichezeshwa na Ahmad Seif wa Pwani ulikuwa wa ushindani kwani kila
mchezaji alijitahidi kuonyesha uwezo wake na kusaidia timu yake kushinda.
No comments:
Post a Comment