Wachezaji
wa Liverpool wakishangilia bao la Daniel Sturridge lililoipa ushindi wa
1-0 dhidi ya Manchester United kwenye Uwanja wa Anfield. Huo ni ushindi
wa tatu mfululizo kwa Liverpool tangu kuanza kwa msimu, matokeo
iliyowahi kupata miaka 19 iliyopita. (Picha kwa Hisani ya Gazeti la
Daily Mail la Uingereza)
Sturridge
akishangilia bao pekee la Liverpool, alilofunga leo. Ushindi huo
umekuja wakati ambao mshambuliaji huyu anaadhimisha miaka 24 ya kuzaliwa
kwake leo Septemba 1.
Sturridge
akidondoka baada ya kupiga kichwa kufunga bao hilo akiunganisha pasi ya
kichwa ya Daniel Agger aliyeunganisha kona ya Steven Gerrard.
Sturridge akikumbatiana na kocha wa Liverpool Brendan Rodgers baada ya kuifungia timu yake bao la ushindi.
Mashabiki
wa Liverpool wakiwa wamekaa jukwaani kuunda picha na kuandika namba 100
ambayo ini idadi ya miaka ambayo nguli wa zamani aliyezaliwa Septemba
2, Bill Shankly ilikuwa aitimize, ingawa alifariki kabla.
Steven Gerrard wa Liverpool, akitunishiana msuli na Robin van Persie wa Man United wakati wa mechi hiyo.
Martin
Skrtel (37), ambaye aliingia kujaza pengo la majeryhi Kolo Toure,
akiruka juu kuwania kupiga mpira wa kichwa kuondoa hatari langoni mwa
Liverpool.
Steven Gerrard akipiga adhabu ndogo.
Kocha
wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson (wa pili kulia) akifuatilia
mtanange huo wa kukata na shoka kwenye dimba la Anfield.
Mshambuliaji Luis Suarez wa Liverpool, akiangalia mechi hiyo akiwa jukwaani.
Kocha wa Liverpool, Rodgers (kulia) na wa Manchester United David Moyes wakitoa maelekeo kwa wachezaji wa vikosi vyao.
BAO pekee la Daniel Sturridge ambaye jana alikuwa
akisherekea siku yake ya kuzaliwa lilitosha kuipa Liverpool ushindi wa bao 1-0
dhidi ya Manchester United kwenye mchezo mkali uliopigwa katika uwanja wa Anfield.
Straika huyo wa kimataifa wa England aliupalaza
kidogo mpira wa kichwa ambao ulikuwa umepigwa na Daniel Agger na kuwapita David
de Gea na Tom Cleverley waliokuwa kwenye mstari wa goli mapema katika kipindi
cha kwanza.
Man United walijaribu kuchomoa bao hilo bila
mafanikio, huku Simon Mignolet akionyesha kiwango safi na kufanikiwa kucheza
mechi yake ya tatu msimu huu bila kuruhusu bao.
Brendan Rodgers alilazimika kubadilisha kikosi chake
cha Liverpool kwa mara ya kwanza msimu huu, kwa kumuweka benchi Kolo Toure ambaye
ni majeruhi na nafasi yake kuchukuliwa na Martin Skrtel ambaye alicheza
sambamba Daniel Agger.
Wayne Rooney alikosekana kwa upande wa Man United
kutokana na majeraha ya kichwa aliyonayo, huku Antonio Valencia pia akianzia
benchi na nafasi zao kuchukuliwa na Ashley Young na Ryan Giggs.
Wachezaji wapya wa Liverpool, Tiago Ilori, Mamadou
Sakho na Victor Moses wote walikuwa jukwaani kuangalia pambano hilo ambapo timu
yao ilianza vizuri na kuandika bao la mapema katika dakika ya nne tu ya mchezo.
Baada ya bao la Liverpool, United walijaribu kusaka
bao la kusawazisha lakini Danny Welbeck na Robin van Persie hawakuwa makini na
kukosa mabao matatu ya wazi na mpaka pambano hilo linamalizika Liverpool 1, Man
United 0.
Katika mchezo mwingine Arsenal waliibuka na ushindi
wa bao 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye pambano kali lililopigwa katika
dimba la Emirates.
Olivier Giroud ndiye alikuwa mfungaji wa bao pekee
la mchezo huo katika kipindi cha kwanza akimalizia krosi safi ya chini chini
iliyopigwa na Theo Walcott kutoka winga ya kulia.
Spurs walijaribu bila mafanikio kuchomoa bao hilo
katika kipindi cha pili huku wakitawala sehemu kubwa ya mchezo huo.
No comments:
Post a Comment