FIFA YAIJIA JUU TUNISIA, YAITAKA KUKAA MBALI NA SOKA
SHIRIKISHO
la Soka Duniani-FIFA limeionya serikali ya Tunisia kuingilia masuala ya
soka baada ya waziri wa michezo wa nchi hiyo Tarek Dhiab kuliomba
shirikisho hilo kuvunja uongozi wa soka wan chi hiyo. FIFA imeiataka
serikali ya nchi hiyo kutoingilia masuala ya shirikisho la soka la nchi
hiyo kwani watalazimika kuifungia nchi hiyo kama sheria zinavyosema.
Hatua hiyo imepelekea Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ali Laarayedh kuitisha
mkutano wa dharura ambao pia utahudhuriwa na wajumbe wa shirikisho hilo
pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya michezo ili kujaribu kutatua
tatizo lililopo. Mapema jana msemaji wa shirikisho la soka la nchi hiyo
amesema kauli ya Dhiab inaweza kuwafanya wakafungiwa na FIFA hivyo
kuzifanya timu zinashiriki michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika na
Kombe la Shirikisho kukosa nafasi ya kuendelea.
No comments:
Post a Comment