KOCHA Mkuu wa Timu ya Yanga, Ernie Brandts, anatarajiwa kuwasili
nchini kesho kutoka Ujerumani, hivyo atakosa kushuhudia mechi ya kirafiki kati ya timu yake na Mtibwa, itakayofanyika leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na LENZI YA MICHEZO, Meneja wa Yanga, Awadhi Salehe, alisema Brandts amemaliza
mafunzo yake ya ukocha nchini Ujerumani, hivyo anarejea kuendelea na majukumu
yake ndani ya Yanga.
Brandts alikuwa nchini Ujerumani akihudhuria mafunzo mafupi
ya ukocha ya siku tatu, yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Barani Ulaya
(UEFA), yaliyoanza Julai 27 na kumalizika Julai 31.
“Tunatarajia kocha atarejea Jumatatu, mimi na
wachezaji wangu tumefurahi sana, japo atakuwa amekosa kushuhudia mchezo huo muhimu
dhidi ya Mtibwa ambao ungemwezesha kupata picha nzima ya kikosi kabla ya kuanza kwa ligi,”
alisema.
Wakati Yanga wakisikitika kumkosakocha wao katika
mchezo huo, wachezaji wa Mtibwa wametamba kuwafunga wapinzani wao na mashabiki wao.
Beki mpya wa Mtibwa aliyesajiliwa kutoka Oljoro JKT, Salim
Mbonde, alisema safu nzima ya ulinzi ya timu yake imejipanga kuhakikisha hakuna
mshambuliaji wa Yanga atakayekatiza mbele yao na kufunga mabao.
"Yanga ni timu kubwa yenye wachezaji wenye viwango vikubwa,
lakini wasitegemee mteremko siku hiyo, beki yetu iko imara na kocha
ametuelekeza namna mbalimbali za kukabiliana na wapinzani wetu,” alisema.
No comments:
Post a Comment