LONDON, England
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger,
amesema endapo mshambuliaji ‘mtukutu’, Luis Suarez, atasajiliwa lazima
atabadilika.
Wenger aliyasema hayo jana, huku
akisisitiza kuwa Arsenal ina miiko na tamaduni zake ambazo kila mchezaji lazima
atazifuata bila kujali yeye ni nani.
"Tuna tamaduni zetu ambazo
tunataka kila mchezaji wetu aziheshimu. Haijalishi yeye ni nani, ametoka wapi. Hii
ni klabu iliyojengeka katika misingi ya heshima na hii si katika kipindi cha
uongozi wangu tu, bali miaka 130 ya klabu. Miiko hii ndiyo ngao ya timu na
lazima iheshimike," alisema Wenger.
Arsenal, imetenga kiasi cha pauni
mil. 40 na moja ya nyongeza ili kumnasa mtukutu huyo aliyefungiwa kucheza mechi 10
kutokana na kitendo cha kumng’ata mchezaji wa Chelsea, Blaslav Ivanovic, pamoja na utovu wa nidhamu.
Hata hivyo Wenger, alikuwa na
kigugumizi alipotakiwa kuthibitisha kama kuna uwezekano wa kumnasa nyota huyo
raia wa Uruguay.
"Sitaki kuongelea suala la Suarez. Hilo
ni suala la Liverpool na Arsenal na tunatarajia kukamilisha kile Liverpool
inachohitaji, na tutakifanya endapo kutakuwa na uwezekano pande zote," aliongeza
kocha huyo.
Lakini kwa upande wa wadau
wamegawanyika, kuna wanaopenda kumuona Suarez akitua Emirates, lakini wengine
wanapinga kiasi cha fedha kulinganisha na mchezaji mwenyewe.
XXXXXXXXXXXXXXXX
Rooney arejea dimbani
MANCHESTER, England
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney, amerejea dimbani, baada ya kuwa nje akiuguza jeraha la paja alilopata mapema Julai, wakati timu yake ikijiandaa na ziara barani Asia.Nyota huyo, usiku wa kuamkia leo, alitarajiwa kuwa kwenye kikosi kilichokutana na Real Betis katika mchezo wa kirafiki wa mwisho kabla ya kuanza msimu mpya.
Kocha David Moyes, alithibitisha kuwa, Rooney atacheza sambamba na Javier Hernandez ‘Chicharito’, Nemanja Vidic, Antonio Valencia na Luis Nani.
Hata hivyo, maisha ya Rooney Old Trafford ni ya utata, baada ya kuonesha nia ya kutaka kujiunga na Chelsea, lakini kocha Moyes amegoma kumwachia, baada ya kukataa ofa mbili za Chelsea, ikiwemo ile ya pauni mil. 23.
No comments:
Post a Comment