MCHEZAJI wa kikapu wa timu ya Golden State Warriors ya nchini Marekani juzi alifanya kliniki ya mchezo huo
iliyofanyika kwenye Viwanja vya Don Bosco, Dar es Salaam.
Curry ambaye timu yake inashiriki Ligi ya NBA pia aligawa
vyandarua 100 kwa kila mchezaji ikiwa ni
mchango wake kwa watoto wan chi za ukanda wa Afrika.
Akizungumza na LENZI YA MICHEZO, Stephen Curry alisema kila pointi
tatu anazofunga kwenye mchezo huo ni vyandarua vitatu anavyochangia.
“Kila pointi tatu ninazofunga kwenye NBA zinachangia
vyandarua vitatu hivyo nafanya ziara barani Afrika kufanya kliniki na kugawa
hivyo vyandarua kwa vijana wanaocheza mchezo huu”, alisema Curry.
Naye Makamu Mwenyekiti wa BFT, Phares Magesa alisema
wanashukuru kwa mafunzo haya kwani yanasaidia kuibua vipaji vvya mchezo huo ila
uhaba vya viwanja ni changamoto kubwa.
“Tunashukuru kutembelewa na wachezaji wakubwa wanaocheza NBA
kwani wachezaji wenye vipaji wanapata nafasi ya kwenda kufanya majaribio NBA na
mwaka huu wanakwenda 13 kufanya majaribio ambapo wengine wanapata nafasi za
kucheza kwenye vyuo nchini Marekani”, alisema Magesa.
Curry ni mfungaji
bora wa timu yake kwa msimu uliopita pia kwa upande wa NBA alikuwa
miongoni wa wafungaji bora watano.
Mchezaji wa mchezo wa kikapu wa Ligi ya NBA, timu ya Golden
State Warriours, Stephen Carrey akifanya mazoezi kwenye kliniki ya mchezo huo
iliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Don Bosco, Dar es Salaam.
|
No comments:
Post a Comment