5. Dimitar Berbatov: Hasara dola mil. 33
Alitoka Tottenham
Hotspur kwenda Manchester United kwa gharama ya pauni milioni 38.
INAELEZWA kwamba
wakati Kocha Sir Alex Ferguson
alipomnunua mchezaji huyo bora wa mara zote nchini Bulgaria mwaka 2008, kila mmoja alitarajia kuwa
amenunua silaha ambayo ingeweza kumsaidia
katika harakati zake za kusaka ubingwa.
Hata hivyo ni kwamba
baada ya Berbatov kutua kwenye klabu hiyo ya Old Trafford akawa mzigo kiasi cha
kuwachefua mashabiki wa timu hiyo.
Hii inaelezwa ni
kutokana na kuwa nyota huyo wa zamani wa
Bayer Leverkusen, tofauti na ilivyotarajiwa na wengi, hakuweza kuonesha
cheche zake kabisa.
Katika kipindi
ambacho mchezaji hiyo amewachezea mashetani wekundu, inadaiwa msaada wake
ulikuwa ni mdogo mno tofauti na alivyokuwa miaka ya nyuma kabla ya kujiunga na
klabu hiyo ya Old Trafford.
Kwa kukosa kutoa
msaada ipasavyo, ikalazimu Manchester United kumuuza kwa hasara kwa
Fulham kwa gharama ya pauni milioni 5.
Mbali na kuuzwa kwa
hasara mwaka 2012, nyota huyo
mwenye umri wa miaka 31 baada ya kusaini
tena mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ya Craven Cottage, lakini nyota huyo wa zamani wa timu ya CSKA Sofia
hadi sasa amefanikiwa kufunga mabao 15
katika kipindi chote alichojiunga na
Fulham.
4.
Lilian Thuram:
Hasara dola mil. 36.5
Alitoka Parma kwenda Juventus kwa gharama ya pauni milioni 41.5.
Mwaka 2001, Thuram alijiunga na klabu ya Juventus akiaminika kama mmoja wa wachezaji wenye misuli ulimwenguni.
Mbali na hilo, nyota huyo alikuwa akiaminika kama beki kisiki alipokuwa akisimama kwenye nafasi ya beki wa kushoto ama beki wa kati kutokana na uwezo wake wa kutopitika kirahisi.
Uwezo huo unadaiwa kufanya hadi sasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 41 kuwa bado miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwa gharama kubwa.
Akiwa sambamba na nyota wengine kama Fabio Cannavaro, Gianluca Zambrotta na Jonathan Zebina, aliweza kujijengea jina nchini Italia katika kipindi cha mwaka 2004 na 2006.
Nyota huyo ndiye aliyeiwezesha timu hiyo kutwaa mataji mawili kati ya manne ya Ligi Kuu ya Serie A, kabla ya kuondoka mwaka 2006.
Hata hivyo, baada ya kipindi cha miaka mitano aliyokipiga kwenye klabu hiyo akajikuta akiuzwa kwa hasara ya pauni milioni 5 kwa Barcelona.
Baada ya kujiunga na na Barcelona, mzaliwa huyo wa kitongoji cha Guadeloupe aliweza kucheza mechi 41 kwa vinara hao wa Catalan kabla ya uwezo wake kuporomoka na kumfanya atundike daluga.
3. Ronaldo: Hasara mil. 37.5
Alitoka Inter Milan kwenda Real Madrid kwa gharama ya pauni milioni 45
Siku ya kwanza tangu atue nchini Hispania, jezi ya Ronaldo ilikuwa ikiuzwa karibia kila mtaa wa mji huo.Inaelezwa kuwa ‘El Fenomeno’ alikuwa ni mchezaji ambaye kila shabiki wa timu alitamani kumuona.
Inaelezwa pia kutokana na uwezo wake, mshambuliaji huyo ambaye alikuwa tishio ulimwenguni ilishuhudiwa akipachika mabao 83 katika mechi 127 alizocheza katika kipindi alichokuwa kwenye uzi wa Real Madrid.
Akiwa na nguli wengine kama David Beckham, Zinedine Zidane na Raul, kinara huyo aliweza kujitengenezea jina vilivyo kwenye timu ya Taifa ya Brazil na kwenye kikosi hicho kinachokipiga kwenye michuano ya La Liga kabla ya kukumbwa na majeraha na matatizo ya unene na kisha baada ya kusajiliwa Ruud van Nistelrooy akajikuta akiondoka taratibu kwenye mipango ya kocha, Fabio Capello na hivyo baada ya kuchekecha kichwa akaona ni bora aombe uhamisho wa kwenda kukipiga AC Milan akiwa na dhamira ya kuimarisha soka lake.
Hata hivyo, kutokana na matatizo aliyokuwa nayo haikuwa rahisi kumuuza kwa bei inayostahili, kwani iliilazimu Real Madrid kumuuza kwa AC Milan kwa gharama ya pauni milioni 7.5.
Pamoja na kuomba kuondoka ilishuhudiwa uwezo wa Ronaldo ukizidi kushuka na huku wingi wa kilo ukizidi kuongezeka na kumfanya akose kabisa uwezo wa kuziona nyavu kama alivyokuwa awali.
Tatizo hilo lilimfanya Ronaldo afunge mabao tisa tu kati ya mechi 20 alizoichezea timu hiyo kabla ya kurejea nyumbani kwao Brazil.
2.
David Villa: Hasara dola mil. 37.9
Inaelezwa kuwa klabu zote kubwa Ulaya zilikuwa zikimfuatilia mfungaji huyo wa mara zote nchini Hispania, baada ya kumshuhudia akifunga mabao 28 katika msimu wake mmoja aliokipiga katika timu ya Valencia.
Ni katika kipindi hicho ambacho Villa aliweza kuzikataa ofa za timu za Chelsea, Liverpool na Tottenham na badala yake akasaini mkataba wa miaka minne na Barcelona.
Kama ilivyo kwa wachezaji wenzake, nyota huyo wa zamani wa Valencia, baada ya kujiunga na vinara hao wa Catalan aliweza kuendeleza wimbi lake la kupachika mabao, lakini baada ya kuibuka Lionel Messi akajikuta akianza kushindwa kuonesha cheche zake.
Ni katika kipindi hicho ambacho Villa alijikuta hana jinsi Barça, licha ya kuwa wakati mwingine mara moja moja aliweza kupata nafasi ya kupachika mabao.
Hata hivyo, baadaye ikashuhudiwa nafasi ya kupewa kucheza kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ya Nou Camp ikiyeyuka taratibu, baada ya kukumbwa na majeraha pamoja na kupandishwa nyota kutoka timu ya watoto.
Hali hiyo inadaiwa ndiyo ikailazimu Barcelona kumuuza kwa Atlético Madrid kwa thamani ya pauni milioni 2.1.
Alitoka Inter Milan kwenda FC
Barcelona kwa gharama ya pauni milioni
69.5.
Zlatan Ibrahimović alilazimika kusajiliwa kwa bei mbaya ili kumpeleka nchini Hispania, ikiwa ni baada ya kutakata akiwa na klabu hiyo ya Nerazzurri.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya nyota huyo kuingia msimu wa mwisho wa kuitumikia klabu hiyo ya mjini Milan na hivyo Barça kulazimika kuongeza uzito kwa kumtumia Samuel Eto’o, ili iweze kumnyakua mfungaji huyo bora wa michuano ya Ligi ya Serie A.
Katika makubaliano ya awali, Barcelona ilikuwa ikimtaka nyota huyo kwa pauni milioni 46 pamoja na nyongeza ya Samuel Eto’o na nyingine ya Alexander Hleb, ambayo ingempeleka kwa mkopo.
Lakini hata hivyo makubaliano hayo hayakufikiwa na badala yake Barcelona ikajikuta ikiingia gharama ya pauni milioni 69.5 na nyongeza ya Eto’o.
Hata hivyo pamoja na kusajiliwa kwa bei hiyo kubwa, mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa ya Sweden alifanikiwa kufunga mabao 16 katika kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kushindwa kuelewana na kocha Pep Guardiola na hivyo baadaye kulazimika kukwea pipa na kurejea nchini Italia, baada ya FC Barcelona kumuuza kwa AC Milan kwa gharama ya pauni milioni 24.
Agosti 2010, nyota huyo wa zamani wa timu za Juventus na Inter ndipo alipojiunga na AC Milan kwa mkopo, lakini kwa makubaliano ya kwamba angepewa mkataba wa kudumu mwishoni mwa msimu.
Akiwa na timu hiyo, aliweza kufunga mabao 21 katika mechi 41 alizocheza na ndiyo yakamsaidia kupata mkataba wa kudumu wa kuitumikia klabu hiyo ya Rossoneri kuanzia Julai 18, 2011 uliokuwa na thamani ya pauni milioni 24.
No comments:
Post a Comment