LONDON, England
KOCHA Manuel Pellegrin ameelezea
kufurahishwa alivyoanza kibarua chake
Manchester City, baada ya kuibuka
na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya
Newcastle katika mechi yake ya kwanza ya michuano ya Ligi Kuu ya England.
Hata hivyo pamoja na kuanza vizuri, kocha
huyo mpya Man City alikataa kusema kuwa kikosi chake tayari kimeshakuwa mmoja
wa timu pinzani katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu licha kuonesha
kiwango kizuri.
Katika mechi hiyo iliyopigwa usiku
wa kuamkia jana alikuwa ni David Silva ambaye alipachika bao la kuongoza dakika
ya sita kabla ya Sergio Aguero, Yaya Toure na
Samir Nasri kuzifumania nyavu za
Toon ambayo nyota wake, Steven
Taylor alitolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu kabla ya timu hizo kwenda
mapumziko.
Akizungumzia ushindi huo, Pellegrini
alisema: "Huu ni mwanzo mzuri na kwa kuwa tumeshinda ugenini tunataka
kuendelea kucheza vizuri.
"Sisi hatukuwa na lengo moja ama mawili bali
tulidhamiria kufanya vizuri zaidi,
lakini kwa sasa hatuwezi kujilinganisha na Manchester United ama Chelsea ambazo
nazo zimeshinda kwani bado ni mapema,”alisema kocha huyo.
Akizungumzia kuhusu mchezaji wake,
Vicent Kompany ambaye aliumia dakika za mwisho za mchezo huo, majeraha ambayo
yanasadikika kuwa ya nyama za misuli ya
paja Pellegrini, alisema kuwa nyota huyo huenda akakaa bechi kwa muda wa wiki
moja ama mbili.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Moyes amtabiria makubwa Van Persie
LONDON, England
KOCHA wa Manchester United, David Moyes amemtabiria makubwa mshambuliaji wake, Robin Van Persie akisema kuwa kuna mambo mengi mazuri yanakuja kutoka kwa nyota huyo.Msimu wa 2011-12, Van Persie aliifungia Arsenal mabao 30 kwenye michuano ya Ligi ya England na kisha msimu uliopita akaifungia Manchester United mabao 25 yaliyomfanya apewe kiatu cha dhahabu kinachotolewa kwa mfungaji bora wa ligi kila mwaka.
Alipohojiwa kama Van Persie anaweza kuvuka mafanikio aliyoyapata katika msimu wake wa kwanza akiwa Manchester United, Moyes alisema: "Nina matumaini anaweza kufanya hivyo.
"Mabao aliyofunga dhidi ya Swansea ni zaidi ya mabao ambayo yamewahi kufungwa na wafungaji bora na kwa jinsi unavyoweza kuona kuna vitu tofauti amevifanya,”alisema kocha huyo.
.
No comments:
Post a Comment