KWA
hakika mpira wa miguu ni biashara kubwa kwa sasa duniani.
Matajiri
wengi kwa sasa wamewekeza katika mchezo huo unaopendwa na wengi na hiyo
inachangia kuufanya upendwe zaidi.
Wachezaji
wa mchezo huo wanahusudu zaidi fedha kuliko kitu kingine na aghalabu mchezaji
kukaa katika klabu moja ilhali kuna klabu ambayo inaweza kumlipa zaidi ya hapo
alipo.
Roman
Abramovich ni mmoja kati ya matajiri wakubwa wanaomiliki klabu ya Chelsea ya
nchini England.
Abramovich si rafiki wa kweli hata kidogo,
amewahi kuwatimua makocha nane waliokuwa wakiifundisha timu hiyo.
Makocha
wapo kwa ajili ya kutimuliwa, lakini hiyo hutokea pale mafanikio
yanapokosekana. Kwa wengine huwa raha mustarehe na hufurahia maisha. Sir Alex
Ferguson ni mfano mzuri kwa Manchester United, kwani ameweza kudumu katika
klabu hiyo kwa miaka 27 kuanzia mwaka 1986 hadi 2013 hadi alipoamua kujiweka
pembeni.
Wakati
mwingine fedha ina jeuri na inaweza kuamua kila kitu, ingawa kuwa nazo wakati
mwingine si njia ya kupata kile unachohitaji katika maisha.
Angalia
jeuri ya pesa, tajiri Roman Abramovich alivyowatimua kazi Claudio Raineri, Jose
Mourinho, Avram Grant, Lusi Felipe Scolari, Carlo Ancelotti, Andre Villas-Boas,
Roberto Di Matteo.
Hivi
ndio fedha inavyofanya kazi katika mpira wa miguu, yote hii ni katika kusaka
mataji.
Kazi
sasa imerudi kwa Jose Mourinho ‘The Special One’ ambaye aliwahi kutimuliwa na
tajiri huyo, amerejea tena Stamford Bridge kukinoa kikosi hicho.
Haya
ndio maisha yalivyo katika mpira wa miguu, yamejaa kila aina ya vituko lakini
ndivyo yanabadilisha maisha ya watu na kuyaboresha.
Hii
ni biashara kubwa kwa kuwekeza na inalipa.
Wapo
wachezaji waliotoka katika familia za kimaskini barani Afrika, waliopata
utajiri kupuitia mchezo huu, tena ni watu wa kuheshimika si Afrika pekee, bali
ni duniani kwa ujumla.
Wana
fedha za kutosha, tena siku hizi wanawajali na wenzao kwa kuwekeza katika vituo
vya michezo ‘Academy’.
Kwa
kweli wanakumbuka kule walipotoka, ni jambo zuri na linapaswa kuigwa na wachezaji
wengine hasa wa Tanzania.
Lakini
ni safari ndefu sana kwa wachezaji wetu wa Tanzania wanahitaji kupitia ili
kufikia huko na kutimiza ndoto za namna hii, kwa sasa ni wachezaji wawili pekee
ambao angalau unaweza kusema wanaweza kutimiza ndoto hizo, Mbwana Samatta na
Thomas Ulimwengu wanaocheza soka la kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Lakini
wakati fulani niliwahi kusikia kuhusiana na Renatus Njohole Foundation, bado
mpango huu haujaimarika, lakini nadhani ni njia nzuri ya kusaidia wengine.
Kwa
kweli fedha zinaamua maisha ya wachezaji, Samuel Etoo ‘Fills’ aliondoka Inter
Milan na kujiunga na Anzhi Makhachkala
ya nchini Russia kwa kuangalia fedha, wakati mwingine mchezaji huangalia fedha
kwanza na mengine yatafuatia baadaye.
Fedha
ndio huamua maisha ya mchezaji, lakini baadaye ya mshiko ni mataji, ndio maana
Abramovich aliwatimua makocha kwa kuwa alikuwa akihitaji kitu kingine baada ya
fedha.
No comments:
Post a Comment