Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, August 4, 2013

NYOTA WATANO AMBAO MISHAHARA YAO KUFURU ULAYA

MADRID, Hispania
MISHAHARA ya wachezaji ni kati ya mambo ambayo yamekuwa yakijadiliwa mara kwa mara, huku baadhi ya mashabiki wakidai wanalipwa fedha nyingi ambazo hawastahili kutokana na kwamba soka ni mchezo wa starehe.

Hata hivyo pamoja na madai hayo, wachezaji hao wameendelea kulipwa fedha nyingi na ifuatayo ni orodha ya wachezaji watano ambao mishahara yao haikamatiki.

5. Neymar - Barcelona 
Mshahara wake kwa mwaka ni pauni mil
17.1
Kwa sasa nyota huyo wa Brazil ameongezeka thamani tangu alipokuwa na uhakika wa kuchezea Brazil kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwakani.

Inaelezwa kuwa nyota huyo mbali na mshahara anaingiza fedha nyingi kutoka kwenye mikataba na wadhamini kama vile Kampuni ya Nike na kwa sasa, Neymar anajiandaa kukinga fedha nyingi zaidi baada ya msimu huu kujiunga na  Barcelona.

4. Samuel Eto'o - Anzhi Makhachkala
Mshahara wake kwa mwaka ni pauni mil
20.5
Raia huyo wa Cameroon, anaripotiwa kuwa mchezaji ambaye analipwa fedha nyingi duniani.

Ukiondoa mikataba ya biashara, mshahara anaolipwa na klabu yake unasadikika kuwa zaidi ya dola milioni 20 ukishaondoa kodi.

Nyota huyo wa zamani wa Barcelona, kwa sasa anasemekana kuwa matawi ya juu Ulaya tangu alipojiunga na timu ya Ligi ya Europa, Anzhi Makhachkala mwaka 2011.

3. Cristiano Ronaldo - Real Madrid
Mshahara wake kwa mwaka ni pauni mil
25.7.
Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Ureno,  ndiye anayeshikilia rekodi ya usajili kutokana na ada ya pauni milioni 80 zilizomuhamisha kwenda Real Madrid  akitokea Manchester United.
Hata hivyo pamoja na kushikilia rekodi hiyo, nyota huyo anashika nafasi ya tatu kwenye orodha hii.
 Inaelezwa kwamba, udhamini wake wa Kampuni za Giorgio Armani na Nike unamfanya mshahara wake kutotetereka.
 
2. Lionel Messi - Barcelona
Mshahara wake kwa mwaka ni pauni milioni
30
Messi anamzidi Ronaldo, kwani ndiye anayeshika nafasi ya pili kwenye orodha ya wachezaji watano wanaolipwa fedha nyingi.

Hata hivyo, tuhuma zilipomuandama ilionekana pauni milioni 30 anazolipwa kwa mwaka si lolote wakati, Messi akishutumiwa kukwepa kodi.
 
1. David Beckham - Amestaafu
Mshahara wake kwa mwaka zilikuwa ni pauni milioni 30.8
Cha kushangaza ni kwamba, Beckham bado anashikilia nafasi ya kwanza licha ya mshahara wake wa miezi mitano aliokuwa akilipwa PSG kuugawa kwenye mfuko mmoja wa hisani mjini Paris.
Kwa mwaka mzima sasa nyota huyo ambaye aliibukia Manchester United, amekuwa akijihusisha na shuhghuli zake binafsi, baada ya kutumia muda wake mwingi akicheza soka kwenye mataifa manne tofauti na kuweza kutwaa mataji kadhaa.



No comments:

Post a Comment