Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, August 1, 2013

MTANZANIA AIBUKA BINGWA KATIKA MASHINDANO YA KURUKA KAMBA NCHINI MAREKANI

hqdefault
 Na Jennifer Chamila-MAELEZO
KIJANA wa Kitanzania Hamisi Kondo (pichani) aibuka mshindi wa dunia katika mashindano ya kuruka kamba yaliyo fanyika Orland Marekani Julia 5 hadi Julai 13 mwaka huu.
 Mashindano hayo yalihusisha nchi kumi na nne zikiwa na wachezaji 480 huku  Bara la Afrika likiwakilishwa na Tanzania, Kenya na Afrika ya Kusini ambapo  kijana  Hamisi  mwenye  umri wa  miaka 14 Mtanzania  aliweza kujinyakulia ushindi huo.
Kijana huyo ambaye ni yatima aliyelelewa na kituo cha kulelea  watoto  yatima  cha  Dogodogo Center  kilichopo jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya mchezo wa kuruka kamba   kituoni  hapo  na baadae kupata ufadhili kutoka kwa Bwana  na  Bibi  Amy Canady nchini Marekani ambako aliweza kusoma na kuendeleza kipaji chake.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam  Hamisi amezungumzia mafanikio yake na kuwaasa vijana wenzake kutokata tamaa  ya maisha kwa kuwa na juhudi ya kupambana ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
“Nawaomba watoto wa mtaani na yatima kutokata tamaa ya maisha kwani hata mimi nilikuwa kama wao na  nimeweza kufanya juhudi na kufanikiwa”alisema Hamisi.
Naye Mkurugenzi  Msaidizi  wa Idara ya  Maendeleo  ya Michezo ,kutoka  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Bi. Juliana Yassoda aliwaomba vijana kutong’ang’ania michezo mikubwa   kama mpira wa miguu kwani kuna michezo midogo midogo ambayo wanaweza kucheza na kufanikiwa kama ilivyo kuwa kwa  Hamisi.
Pia Mwenyekiti wa Kituo cha Kufundisha Michezo Tanzania (TSTC), Bw.Dennis Makoi ambaye alishirikiana na kituo cha dogodogo kumtafutia ufadhili Hamisi nchini Marekani,ametoa shukrani zake za dhati kwa familia ya Bw. na Bi.Amy Canady wa huko Marekana  kwa ufadhili  na kusaidia kufanikisha ushindi huo.
 Hivi sasa Hamisi anaendelea na masomo nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment