Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, May 18, 2013

YANGA YABEBA MWALI WAKE KWA SHANGWE BAADA YA KUIFUNGA SIMBA BAO 2-0


Wachezaji wa Yanga na mashabiki wakiwa na kombe

Mashabiki wa Yanga wakiwa hawaamini kilichotokea

Mwamuzi Martin Saanya akipatiwa huduma ya kwanza

Mshambuliaji wa Simba akiwa amebebwa na mashabiki wa Yanga ambao waliondoka naye

Shabiki wa Yanga akishangilia kwa staili ya aina yake 

Shabiki wa Yanga akipelekwa kupewa huduma ya kwanza baada ya kuzimia wakati mchezo ukiendelea.

Beki wa Yanga David Luhende akiondosha mpira kwenye himaya ya mshambuliaji wa Simba Amri Kiemba


Yanga ya Dar es Salaam leo imetwaa taji la 24 la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara bara ya kuifunga Simba mabao 2-0 kwenye mchezo wa kufunga pazia la Ligi uliochezwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Yanga inamaliza msimu wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 60, ikifuatiwa na Azam FC yenye 52 na Simba 45 
Mchezo huo ulianza kwa kasi ambapo Yanga walifanikiwa kupata bao la kwanza lililofungwa na Didier Kavumbangu dakika ya tano kwa kichwa ambalo lilidumu hadi mapumziko.

Simba ilipata nafasi ya kusawazisha dakika ya 27 baada ya Mrisho Ngassa kuangushwa kwenye eneo la hatari na Nadir Haroub na ndipo mwamuzi Martin Saanya kuamuru penalti, lakini mkwaju wa Mussa Mudde dhaifu ulipanguliwa na Ally Mustafa ‘Barthez’ kabla ya kipa huyo kuuchupia na kuudaka.

Kipindi cha pili, Simba SC walikianza vizuri dakika 10 za mwanzo wakipeleka mashambulizi langoni mwa Yanga kutokea pembeni, lakini safu ya ulinzi ya mabingwa hao wa Bara ilisimama imara kukabiliana na hatari zote.

Dakika ya 62 Hamis Kiiza aliunganisha krosi maridadi ya Simon Msuva na kuipatia Yanga bao la pili. Baada ya bao hilo, Yanga walianza kucheza kwa kujiamini zaidi na Simba wakionekana kucheza ili kutoruhusu mabao zaidi.

Mwamuzi Saanya dakika 87 aligongana na mchezaji na kuchanika kichwani  wakati anakwenda kuamua ugomvi kati ya Didier Kavumbangu na Nassor Masoud ‘Chollo’ akaanguka na kutibiwa kwa dakika hadi kuinuka dakika ya 90 na kumaliza mpira baada ya sekunde kadhaa.

Mchezo huo uliochezeshwa na Martin Saanya wa Morogoro, akisaidiwa na Samwel Mpenzu wa Arusha na Jesse Erasmo kutoka Morogoro, na mezani alikuwepo Hasim Abdallah wa Dar es Salaam.

Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Haruna Shamte, Mussa Mudde, Shomary Kapombe, William Lucian ‘Gallas’, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Abdallah Seseme/Ramadhani Singano ‘Messi’, Amri Kiemba/Jonas Mkude na Haruna Chanongo/Felix Sunzu.

Yanga SC, Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite/Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan,  Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Didier Kavumbangu na Hamisi Kiiza/Niaar Khalfan.

No comments:

Post a Comment