IDADI ya
mabondia wa timu ya taifa walioripoti mazoezini, imeongezeka na kufikia 10
badala ya 16 walioitwa kuunda kikosi hicho.
Timu hiyo
ilianza mazoezi katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Jumanne ya wiki
iliyopita, ambapo mabondia wanne pekee ndio walikuwa wameripoti mazoezini kwa
wiki hiyo.
Lenzi ya Michezo jana ilishuhudia mabondia 10 wakifanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na
michuano ya kimataifa, ikiwemo ile ya Afrika wakati idadi hiyo ikitarajiwa
kuongezeka zaidi ifikapo wikiendi hii.
Kocha
Mkuu wa timu hiyo, Lemmy Ngabo amesema kuwa mabondia wengi ambao ni waajiriwa
wa Taasisi mbalimbali zikiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wameshapewa kibali
cha kujiunga na timu hivyo kufikia Jumatatu huenda mabondia wote 16 wakawepo
mazoezini.
Lemmy
alisema kwa sasa timu hiyo itafanya mazoezi katika uwanja wa ndani hadi hapo
itakapofika programu ya kwenda ufukweni na baadaye gym.
“Kufikia
Jumatatu tunatarajia mabondia wote watakuwa wamewasili mazoezini na tutaendelea
kufanya mazoezi katika uwanja wa ndani hadi hapo tutakapofikia wakati wa
kujenga nguvu kwa mabondia pamoja na viungo, ambapo tutalazimika kuhamia katika
fukwe na gym,” alisema Lemmy.
No comments:
Post a Comment